Thursday, 23 June 2016

RIHANNA ATOKWA NA MACHOZI KATIKA TAMASHA CHANZO HIKI HAPA

SUBSCRIBE HAPA ILI USIPITWE NA VIDEO KALI KILA SIKU HAPA 
https://www.youtube.com/watch?v=8hLupLJKJsw
Nyota wa muziki Rihanna alibubujikwa na machozi wakati wa tamasha mjni Dublin usiku wa kuamkia jana baada ya kuwasili akiwa amechelewa kwa dakika 30 katika ukumbi huo.
Mwanamuziki huyo alijawa na hisia wakati alipoanza kuimba wimbo wa 'Love The Way You Lie' aliyoimba kwa ushirikiano na mwanamuziki Eminem.
Mashabiki waliweka picha na video za mwanbamuziki huuo katika mitandao ya kijamii wakionyesha wasiwasi wao kuhusu kile kilichotokea.
Rihanna hakuelezea ni nini kilichotokea mbali na kuandika ujumbe kwatika mtandao
wake wa Instagram akiusifu usiku huo,ilikuwa tamasha iliojaa hisia kwambgu,aliandika.
''Nina bahati kuwa na kikosi kama vile #Navy man,nimebarikiwa.Ninashukuru sana kwa kuwa nanyi nyote''.#DUBLIN#ANTIWORLDTOUR''
Rihanna atakuwa nchini Uingereza katika uwanja wa Webly siku ya Ijumaa.Wakati alipozindua albamu hiyo ,alionekana akiangalia kando na kamera na kuinua mikono kama ishara ya kutaka kujizatiti.
Lakini mashabiki wake waliokuwa wamefurika katika tamasha hilo waliendelea kumuimbia hadi akafuta machozi yake na kuendelea na dakika 80 za kuwatumbuiza.
''Sijawahi kusikia watu wakipiga kelele kwa sauti ya pamoja na hilo limetokea Ireland mjini Dublin'',aliuambia umati.

No comments:

Post a Comment

advertise here