Friday, 1 April 2016

MABESTE NA LISA KUFUNGA NDOA MWEZI WA NANE

LAYIII
Rapper Mabeste amesema anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake wa siku nyingi, Lisa aliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Kendrick.
Akiongea katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, Mabeste alisema:

“Hivi karibuni na Mama watoto wangu Lisa tumetoka kuwaona wazazi wake na kuna taratibu nimepatiwa vitu vingine zaidi watu tutawajulisha. Zaidi nipo katika harakati za kuweka mambo sawa, nadhani hadi mwezi wa nane tutakuwa tunabariki ndoa, yaani mwaka huu ntakuwa busy zaidi na mambo ya ndoa na kazi zangu za muziki.”

No comments:

Post a Comment

advertise here