LAYIII
Mshambuliaji wa kimataifa wa Togo na klabu ya Tottenham Hotspur Emmanuel Adebayor, ambaye kabla ya dirisha la usajili kufungwa alikuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya West Ham United ya Uingereza kwa asilimia kubwa. Moja kati ya wachezaji ambao tulikuwa tukitarajia kuona
wakihama vilabu vyao ni Adebayor.
Licha ya mipango yake ya kutaka kuihama klabu hiyo kushindikana, inaonekana Tottenham Hotspur hawana mpango wa kuendelea na mchezaji huyo wa Togo kwani wamemuondoa katika list ya wachezaji watakao watumia katika michuano ya Europa League.
Hii ni mara ya pili kwa Adebayor kupata wakati mgumu katika klabu ya Tottenham Hospur, kwani mara ya kwanza ilikuwa chini ya kocha Andre Villas Boas ambaye alikuwa hampi nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza hadi kufikia wakati wakakwaruzana.
Adebayor alikuwa ana husishwa kujiunga na vilabu vya Aston Vill na West Ham United, hivyo kuna kila dalili ya huduma yake kuto hitajika na kocha Mauricio Pochettino White Hart Lane, kwani hadi jezi namba 10 aliyokuwa anatumia amepewa Harry Kane.
Licha ya kuwa Adebayor alikuwa na mpango wakubakia London, huenda akatimkia Qatar
ambako dirisha la usajili bado halijafungwa ili apate nafasi ya kucheza
na kulinda kipaji chake, kwani karibia kila nchi barani Ulaya
imeshafunga dirisha la usajili.
No comments:
Post a Comment