Monday, 17 August 2015

UKAWA na Zanzibar, Sumaye kumnadi Magufuli, ACT Wazalendo watoswa mgombea Urais + alidai vifaa baada ya kubwagwa kura za maoni!? (Audio)

tues
Magazeti ya August 18 2015 tayari yako mtaani, nimezinasa zile zote kubwa kubwa za leo magazetini @CloudsFM zikiwa na baadhi ya stori hizi kubwa…
Mgombea Urais aliyependekezwa na kuchukuliwa fomu kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Prof. Kitila Mkumbo aikataa fomu ya ugombea Urais kupitia Chama hicho akisema kuwa kwa sasa hayuko tayari kugombea nafasi hiyo.
UKAWA imetangaza mgawanyiko wa Majimbo 253 kati ya 265 ya Ubunge huku 12 yaliyokuwa kwenye mvutano yabaki kiporo na CCM yapitisha majina ya wagombea katika majimbo 9 ya wabunge kati ya Majimbo 11 yaliobaki.
Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye asema atazunguka nchi nzima kumnadi mgombea Urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli dhidi ya mpinzani wake Edward Lowassa na Mafuriko ya UKAWA yaiteka Zanzibar ni mkusanyiko wa watu uliojitokeza kumuunga mkono Lowassa.
Kuna nyingine imesikiaka inayomhusu Mbunge wa Mbinga Mashariki mkoani Ruvuma, Gaudensi Kayombo amabye ameidai CCM vifaa vyake vya kampeni baaada ya kushindwa kura  za maoni… nyingine inahusu mchezo mchafu umebainika kufanywa na wafanyabiashara wa kubwa wa maduka ya kubadilisha fedha ili kuhujumu uchumi wa nchi.
Uchambuzi wote wa magazeti nimekuwekea katika sauti hapa chini, bonyeza play kuisikiliza.

No comments:

Post a Comment

advertise here