LAYIII
Erick Evarist
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) Nape Nnauye amemuumbua waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumwelezea kama mtu
aliyenunua nafasi anayoigombea kwa Chama Cha Maendeleo na Demoktrasia (Chadema).
Erick Evarist
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) Nape Nnauye amemuumbua waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumwelezea kama mtu
aliyenunua nafasi anayoigombea kwa Chama Cha Maendeleo na Demoktrasia (Chadema).
Erick Evarist
KATIBU wa Itikadi na
Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) Nape Nnauye
amemuumbua waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumwelezea kama mtu
aliyenunua nafasi anayoigombea kwa Chama Cha Maendeleo na Demoktrasia
(Chadema).
Akizungumza na gazeti hili juzi, Nape
alisema Lowassa hapendwi na wafuasi wa vyama vya upinzani, isipokuwa
alipewa nafasi hiyo baada ya kuinunua kwa viongozi wanaounda umoja wa
Ukawa, ambao wana tamaa ya fedha.
“Kila mtu anajua kuwa huyu bwana
ameinunua hii nafasi kwa viongozi wa Ukawa, ndiyo maana watu wenye akili
zao, wameamua kujiweka pembeni wamewaachia wenyewe na mzigo wao
usiobebeka, inashangaza kuwa sisi tunawafukuza mafisadi wao wanawapokea,
sasa wakipewa nchi si itakuwa hatari zaidi?” alihoji Nape.
Alisema Lowassa alitumia fedha nyingi
kuwarubuni watu wa Ukawa ili wampe nafasi baada ya kukatwa CCM, ndiyo
maana baada ya kumkaribisha kundini, hakuna tena kiongozi wa Chadema
wala Ukawa anayezungumza kuhusu ufisadi, kwani mlengwa wao mkuu wa miaka
yote kuhusu ufisadi alikuwa Lowassa.
“Hivi umeshawasikia tangu ajiunge nao
wanazungumza kuhusu ufisadi? Wanaona aibu kwa sababu katika nchi hii,
ukitaja fisadi na mafisadi huwezi kumweka kando. Unafikiri Watanzania ni
wajinga kiasi kwamba hawaoni huu usanii?” alihoji Nape.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania
Bara, John Mnyika, wala yule wa Zanzibar Salum Mwalimu hawakuweza
kupatikana kuzungumzia madai hayo, jitihada zinaendelea.
No comments:
Post a Comment