Monday 17 August 2015

SABABU ZA JERRY MURO KUSHINDWA KATIKA KURA ZA MAONI

LAYIII
ina la Jerry Muro sio geni masikioni mwa walio wengi kwani aliwahi kufanya kazi ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa muda mrefu na zilizofanya jina lake kukua na watu kumtambua, Jerry ambaye kwa sasa ni mkuu wa idara ya habari ya klabu ya Dar Es Salaam Young African.
Mwaka 2015 aliamua kuingia rasmi katika siasa kwa kuanza harakati za kutaka kulirudisha jimbo la Kawe kwa chama tawala, Jerry alikuwa ni miongoni mwa makada 21 wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea ubunge wa jimbo la Kawe kupitia kwa chama cha mapinduzi (CCM).
Muro 20150727_001927
Kwa bahati mbaya kura hazikutosha kumuwezesha Jerry Muro kupata ridhaa hiyo ya kupata nafasi ya kugombea ubunge wa Kawe kupitia chama cha mapinduzi, ila ameeleza saba
bu za yeye kukosa nafasi hiyo na nini kilipelekea yeye kushindwa katika kura za maoni, hii ni exclusive interview aliofanya na millardayo.com Jerry Muro ana haya.
DSC_0111
“Kweli nilikuwa mgombea wa jimbo la Kawe kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM nilikuwa miongoni mwa wagombea 21, tukiwa katika mchakato nilipata changamoto mbili ya kufiwa na baba yangu na kuvunjiwa nazi na mayai lakini kubwa ni kufiwa  na baba yangu mzee Muro alifariki tarehe 31 wakati sisi tunaelekea ukingoni wa kuitimisha kampeni na alivyofariki mzee wangu nilisitisha kila kitu”
Hadi sasa Halima Mdee wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ndiye mbunge rasmi wa jimbo hilo hadi pale Oktoba 25 uchaguzi mkuu utakapofanyika wa kuchagua wabunge, madiwani na Rais, Halima Mdee alishinda katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 na kufanya awe mbunge wa jimbo hilo.
Zaidi msikilize Jerry Muro hapa


No comments:

Post a Comment

advertise here