LAYIII
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es
salaam limepiga marufuku wagombea wa vyama vya siasa kufanya vitendo
vinavyo hatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kufanya mikusanyiko
isiyo rasmi kwenye masoko na vituo vya daladala.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova.. ‘Sasa
kuna jambo limejitokeza ambalo limetulazimisha sisi jeshi la Polisi
kupiga marufuku wagombea mbalimbali wa vyama katika uchaguzi huu
hususani wale wenye nafasi ya Urais kwa vitendo vyao au kwa mtindo ambao
umeibuka sasa hivi wa kwanza kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar es Salaam kama vile vituo vya Daladala, Masoko, ndani ya Daladala au
Mabasi yoyote yale – Kova
‘Na hii inasemakana kwasababu ya kujua
matatizo ya watu ambao wenye kipato cha chini inawezekana nia ni nzuri
sana lakini sisi hapa atuzungumzia siasa au Uchumi hapa tunazungumzia
suala la Usalama kutokana na uzoefu uliojitokeza kwa zoezi hilo ni
kwamba hilo zoezi sio la rasmi pia ziara hizo zinasababisha mikusanyiko
mikubwa isiyo ya lazima katika hali ambayo inaashiria kutokuwepo kwa
Amani – Kova
‘Wakati wa
ziara wa aina hizo wamejitokeza makundi tofauti ya watu wakiwemo,
waendesha Bodaboda wengi, watu wa Daladala wengi wanajitokeza sawa
wanashangilia lakini kwa watu wengine ambao wasio wa makundi hayo ni
kwamba inakuwa inaleta taharuki, hofu, usumbufu, kuna kuwa na makelele
mengi, msongamano wa magari, au hata kusimamisha usafiri katika eneo
hilo ambalo mgombea anakuwepo nasema kwamba inawezekana huyo mgombea
kuna faida anayoipata lakini yeye kupata faida peke yake haitoshi kama
suala la usalama alizingatiwa’ – Kova
‘Kwa mfano
leo tarehe 25 mwezi wa nane ilibidi RPC wa kamanda Polisi Mkoa wa
Ilala, Lucas Mkondya alilazimika kukutana ana kwa ana na Mgombea Urais
kupitia Chadema, Edward Lowassa saa sita mchana watu walikuwa wamejaa
pale katika mtaa wa Congo nadhani na Uhuru misongamano ya Magari mengi,
Pikipiki wananchi wakalalamika kwamba ni nini sasa kinatokea na unajua
Dar es Salaam ukisimamisha magari kutokana na kundi lako kubwa basi
litawaathiri Wananchi’ – Kova
Unaweza uka bonyeza Play kumsikiliza Kamanda
No comments:
Post a Comment