LAYIII
Unapowazungumzia mastaa waliojizolea mashabiki wengi Bongo kupitia muziki wa Kizazi Kipya, huwezi kuacha kuwataja Ali Saleh Kiba na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Wasanii hao,
japokuwa ni mahasimu wakubwa wa kutokaa zizi moja, lakini chakushangaza, asilimia fulani ya vitu wanavyofanya vinafanana kiasi cha kuonekana kama mafahari ambao hawakai zizi moja lakini wanakula nyasi zilezile.
MAPENZI
Kwa wakati fulani, mastaa hao ambao wote ni wenyeji wa Mkoa wa Kigoma wakitokea Kabila la Wamanyema, wameonekana kufanana kwenye suala la mapenzi hasa mastaa wa kike wanaotajwa kuwahi kutembea nao kama ifuatavyo;
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Penzi la Ali Kiba na Lulu ambaye ni staa wa Bongo Movies liliibuka mara tu baada ya kifo cha aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Steven Kanumba.
Baada ya hapo, kwa nyakati tofauti uvumi huo ulienea zaidi baada ya Ali Kiba kunukuliwa akimsifia Lulu mbele ya vyombo vya habari kuwa ni wife material (ana sifa za mke) japokuwa hakukuwa na uthibitisho kuhusu uhusiano huo.
Kwa upande wake, Diamond naye aliwahi kutoa kauli tata akidai kuwahi kutoka kimapenzi na Lulu japokuwa mrembo huyo alikataa katakata huku Diamond akikazia kwa kudai kuwa siri ya kutembea na Lulu wanayo waliokuwa wapenzi wake kwa nyakati tofauti, Wema Sepetu na Penniel Mungilwa ‘Penny’.
JOKATE MWEGELO
Uvumi kuhusu Jokate kutoka na Diamond ulienea ghafla kama moto wa kifuu kabla ya wawili hao kumwagana bila sababu za msingi. Kama vile wanaambiana, Ali Kiba naye akatesti zali lake ambapo mpaka sasa anaripotiwa kutoka kimalavidavi na staa huyo wa kike.
UKARIBU NA WEMA
Diamond alikuwa wa kwanza kabla ya Kiba kuwa karibu na Wema Sepetu kiasi cha kuwa wapenzi ambapo inadaiwa kuwa jina la Diamond lilipaa maradufu baada ya kuwa na mrembo huyo. Hata hivyo, mapenzi yao hayakudumu sana kwani baada ya kumwagana na kurudiana mara kadhaa wakamwagana jumla.
Kwa sasa Diamond amezama kwenye penzi la mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ huku asilimia za kurudiana na Wema zikiwa ziro.Bila kulaza damu, Kiba naye akatumia fursa hiyo na kuwa karibu na Wema hasa kwa kutambua nyota kali ya diva huyo mbele ya Watanzania ambapo alitaka naye afanikiwe kupitia nyota hiyo. Inaaminika nyota ya Wema ndiyo iliyompa tuzo 5 za KTMA alizozoa mwaka huu.
KOLABO ZA MUZIKI
Katika kile kinachozidi kuongeza utamu wa vita wa mafahari hao wawili ni uwepo wa kolabo zinazofanana japokuwa Ali Kiba anaonekana kwenda taratibu kidogo katika utekelezaji wake.
KOLABO NA DAVIDO
Diamond alikuwa mjanja wa kwanza kufanya kolabo kali ya Number One Remix na Davido wa Nigeria mapema mwaka jana. Mashabiki wa burudani walishangazwa baada ya Davido naye kuzungumzia wazi kuwa anatarajia kufanya kolabo na Ali Kiba ambapo kolabo hiyo inasubiriwa kwa hamu.
NEYO
Umaarufu wa Diamond ulimfanya akutane na staa mkubwa wa Marekani, Neyo na kufanya naye kolabo ambayo bado haijaachiwa, lakini Kiba naye akapata zali la kurekodi kolabo na staa huyo kupitia shoo maarufu ya Coke Studio. Mashabiki wa staa huyo wanasubiria kwa hamu ukaribu kati yake na Neyo uzae kolabo rasmi ya wimbo ukiachana huo wa Coke Studio.

No comments:
Post a Comment