Friday, 3 July 2015

ULIPITWA NA MAGAZETI YA LEO CHEKI HAPA

LAYIII
Wakati vikao vya juu vya CCM vikikaribia kuanza mchakato wa kumpata mgombea Urais wa chama hicho, mji wa Dodoma umeanza kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.

StoriKUBWA >> Makao Makuu CCM Dom.. Waliosimamishwa Bungeni, Hakimu Feki Mahakamani !!

In Case
MWANANCHI
Wakati vikao vya juu vya CCM vikikaribia kuanza mchakato wa kumpata mgombea Urais wa chama hicho, mji wa Dodoma umeanza kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.
Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Mwananchi kwenye maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma hadi jana, umebaini kuwa tayari nyumba nyingi za kulala wageni na hoteli zimeshajaa.

Baadhi ya wajumbe wa vikao hivyo ni wabunge ambao tayari wako Dodoma wakiendelea na Bunge, wengine ni wapambe wa makada waliokuja kurejesha fomu za kuwania Urais ambao hawajaondoka.
Baadhi ya Mameneja wa hoteli hizo walisema watu hao wataondolewa kuanzia Julai 6 iwapo hawatakuwa miongoni mwa waliopangiwa vyumba, huku kukionekana pia baadhi ya wenyeji wameanza kukarabati nyumba zao kwa ajili ya kupangisha wageni mbalimbali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime amewahakikishia wageni kuwa Jeshi lake limejiandaa vizuri kwa ugeni huo mkubwa utakapoingia, kuishi na hadi kuondoka.
MWANANCHI
Hali tete ndani ya Ukumbi wa Bunge jana iliendelea kutanda wakati Spika Anne Makinda alipolazimika kuahirisha kikao asubuhi kutokana na kelele na baadaye Wabunge saba wa upinzani kuadhibiwa, wakiwamo watano waliozuiwa kuhudhuria hadi kumalizika kwa Bunge la 10.
Hali hiyo ndani ya Bunge iliendelea kwa siku ya pili mfululizo na mara zote kusababisha Spika kuahirisha vikao baada ya shughuli za Bunge kushindwa kuendelea kutokana na kelele za wapinzani wanaopinga kitendo cha kuwasilishwa miswada mitatu kwa hati ya dharura wakidai hakuna haja ya haraka hiyo.
Jana Spika Makinda aliibuka na dawa mpya na kuitumia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwaadhibu wabunge hao saba.
Wabunge John Mnyika, Moses Machali, Tundu Lissu, Felix Mkosamali na Paulin Gekul wamefungiwa kushiriki vikao kuanzia leo hadi Bunge litakapovunjwa Julai 9.
Wabunge wengine wawili, Mchungaji Peter Msigwa na Rajab Mbarouk wamefungiwa kushiriki vikao viwili kuanzia leo baada ya Kamati hiyo kuwatia hatiani wawakilishi hao wote saba kwa kudharau mamlaka ya Spika.
Wengine watatu, Joseph Selasini, Khalifa Suleiman Khalifa na Rajabu Abdalah walitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo leo saa 4:00 baada ya wito wa kuwataka wahudhurie jana kuchelewa.
Mashtaka yetu yaliendeshwa kwa haraka, hatukupatiwa muda wa kutosha kujieleza wala kumtumia wakili,” alisema Machali baada ya Bunge kuahirishwa.
Mbunge Tundu Lissu alisema ni bora kufukuzwa kuliko kuendelea kushuhudia gesi ya Watanzania ikiuzwa kwa nguvu bila ya huruma… Mchungaji Msigwa alisema hata angefungiwa kushiriki vikao vyote, asingeathirika.
NIPASHE
Mtu mmoja Jane Mahanga aliyejifanya hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Sirari, amenaswa na kufikishwa katika Mahakama ya Wilaya Tarime.
Hakimu huyo feki amefunguliwa mashtaka matatu, likiwamo la kujifanya hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Sirari na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, Tshs. Milioni 4, mshtakiwa huyo ametupwa rumande hadi hadi Julai 16.
Kabla ya kutiwa Mbaroni alikuwa amewatapeli watu wengine Lucas Ryoba pesa za vinywaji katika grosari ya Kantini ya Uhamiaji iliyoko Sirari.
Mshitakiwa huyo alikamatwa na kufikishwa katika kituo cha Polisi wilayani hapo na walalamikaji wengi kujitokeza baada ya kudai kutapeliwa na mwanamke huyo, hata hivyo alikana mashitaka yote yanayomkabili lakini aliwekwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini.
Siku moja baada ya CCM, kufunga zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuteuliwa  kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mtangaza nia Dk. Muzzamil Kalokola amerejesha fomu kwa kuchelewa akidai amekwamishwa na msafara wa Rais Jakaya Kikwete.
Dk. Kalokola alirejesha fomu hiyo jana akiwa na wenzake, Mwalimu Anthony Chalamila, Helena Elinewinga na Peter Nyalali mtoto wa Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Hayati Francis Nyalali, walishindwa kurudisha fomu hizo juzi jioni ambao ulikuwa muda wa mwisho.
Nimewaeleza ukweli kwamba nilikwama Morogoro kwa saa zaidi ya nne nikisubiri msafara wa Rais Kikwete upite, ningewezaje kuwahi deadline. Nashukuru Mungu wamenielewa baada ya kubishana kwa muda mrefu… Hata huyo niliyemkabidhi fomu yangu simjui jina, isipokuwa ni Ofisa wa Idara ya NEC na Oganaizesheni Makao Makuu ya CCM Dodoma. Kuna vitu vinashangaza lakini ilinibidi niwaombe wasininyime haki yangu ya kurejesha fomu kwa kuwa niliichukua nikiomba kuteuliwa kugombea”– Dk. Kalokola.
NIPASHE 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya Dar es Salaam, imeendelea na kigugumizi baada ya jana kushindwa kutoa hukumu dhidi ya Mawaziri wa zamani, Basil Mramba aliyekuwa Wizara ya  Fedha na Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja na kuiahirisha hadi wiki ijayo.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya Ofisi na kusababisha hasara ya Shilingi bilioni 11.7 kwa kampuni ya Alex Stewart kufanya ukaguzi wa dhahabu kwenye migodi.
Hukumu ya kesi ya viongozi hao itatolewa Jumatatu ijayo, kwa mujibu wa Hakimu Saul Kinemela, aliyeiahirisha kesi hiyo jana na kueleza kuwa  Mwenyekiti wa jopo la Mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji John Utamwa, anaumwa.
Hukumu ilikuwa itolewe Jumatatu wiki hii lakini ilishindikana kwa maelezo kuwa Hakimu Kinemela alikuwa safarini Dodoma na sasa itatolewa Jumatatu mchana

 



No comments:

Post a Comment

advertise here