Friday, 3 July 2015

ROBOT LINALOTENGENEZA MAGARI LAUWA MFANYAKAZI

LAYIII

ROBOTI LAMUUA MFANYAKAZI KIWANDA CHA MAGARI CHA VOLKSWAGEN UJERUMANI

Hiki ni moja ya viwanda vinavyotengeneza magari aina ya Volkswagen nchini Ujerumani.

Roboti zikichomelea magari katika kiwanda cha Volkswagen.
Hapa ndipo mfanyakazi wa Volkswagem alipofariki kwa kuuawa na roboti kaskazini mwa jiji la Frankfurt, Ujerumani.
Frankfurt, Ujeruman
ROBOTI moja iliyokosa mwelekeo imemuua mfanyakazi mwenye umri wa miaka 22 katika kiwanda cha kutengeneza magari cha Volkswagen nchini Ujerumani.
Tukio hilo linaaaminika kuwa la kwanza katika vifo vyenye kusababishwa na roboti za viwandani, jambo ambalo wataalam wamelikanusha kwamba lina mwelekeo huo.
Wataalam wamesisitiza kuwa tukio hilo ni moja ya makosa ya binadamu na si makosa ya roboti yaliyosababisha kifo cha mfanyakazi huyo kwenye kiwanda cha Baunatal, karibu na Kassel, Ujerumani ya kati ambako wafanyakazi 15,000 wameajiriwa kuunganisha ‘giaboksi’.

 


No comments:

Post a Comment

advertise here