Wednesday, 18 March 2015

kiba kutambulisha style yake ya cheketua

GOOD News ni kwamba, mfalme wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba ‘Mwana Dar Live’ ameshafuta kiti chake na Aprili 5, mwaka huu (Sikukuu ya Pasaka) ndani ya Uwanja wa
Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar anatarajiwa kutambulisha staili yake mpya ya Chekecha Cheketua.
Mkali wa Bongo fleva, Alikiba.
Staili hiyo atakayoitambulisha Mwana Dar Live imetokana na wimbo wake mpya unaobamba kila kona wa Chekecha Cheketua.
Kufunika Dar Live
Kuonesha kuwa utakuwa ni usiku wa Mwana Dar Live, atahakikisha kila atakayefika mapema anapata nafasi ya kupiga naye picha kwenye ‘red carpet’ sambamba na kuchonga naye mawili-matatu huku akigawa zawadi kutoka kwa waandaaji wa shoo hiyo kwa watu  watakaopendeza.
KUPIGA ZOTE KALI
Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa Mwana Dar Live kufanya shoo ya kufa mtu ilikuwa ni mwaka 2013 ambapo aliwapagawisha mashabiki kwa ngoma zake kali zisizochuja kama Dushelele, My Everything, Single Boy na nyingine nyingi.
Mwana Dar Live amerudi upya akiwa na ngoma mpya kabisa zinazotikisa kama Mwana, Kimasomaso pamoja na Chekecha Cheketua ambayo ni habari ya mjini.
Mashabiki pia wajiandae kwa sapraizi kibao kutoka kwa Ali Kiba ikiwa ni pamoja na kuwaonjesha ngoma zinazobamba alizofanya na mdogo wake wakiwa kama Kiba Square ambazo ni Kidela, Pita Mbele n.k
MASHAUZI CLASSIC NDANI
Ili kukamilisha shoo ya Mwana Dar Live, kwa wale mashabiki wa muziki wa Mwambao watakata kiu na kundi zima linalosumbua kwa sasa la Mashauzi ClassicMashauzi watakamua jukwaani vilivyo huku wakiongozwa na Isha Mashauzi ama Malkia wa Masauti kama anavyopendwa kujiita.
Mashabiki wategegemee kusikia ngoma kali kutoka kwake kama vile Mama Nipe Radhi, Nimlaumu Nani, Mapenzi Hayana Dhamana na nyingine nyingi.Kama hiyo haitoshi Mashauzi Classic watawapagawisha mashabiki na albamu ya tatu ijulikanayo kama Asiyekujua Hakuthamini.
Msaga Sumu
Kama ilivyo kawaida yake, siku hiyo atakusanya ‘kijiji’ jukwaani na kuimba nao pamoja ngoma zake zote kali kama vile Kijoti Joti huku mashabiki wa Simba na Yanga wakipata ladha ya kipekee kwa wimbo unaotikisa katika shoo ya Vigodoro wa Naipenda Simba na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment

advertise here