Wednesday, 18 March 2015

Hii Good news kutoka kwa rapper Fid Q kashea na sisi iko hapa…

.
.
Good news ninayokusogezea ni hii inamuhusu rapper Fareed Kubanda ambaye leo hii amekabidhiwa tuzo ya Champion of the 2015 European year for development in
Tanzania kutoka umoja wa nchi za Ulaya.
 Akiongea kwenye Amplifaya:..’Tarehe hii ya leo ambayo ni 17 machi ikiwa siku ya Jumanne nina furaha sana kwasababu ni siku ambayo nimepewa tuzo ya CHAMPION of the 2015 European year for developement, lakini nimepewa kwasababu nilikuwa natenga muda wangu kukaa na kuzungumza na jamii, kwa mfano nilishawahi kufungua darasa la Ujamaa Hip Hop ambalo sasa linabidi nilirudishe tena, nilikuwa natoa elimu kwa vijana mbalimbali wa mitaani na wengineo wanaojihusisha na mihadarati lakini ndani ya mwezi mmoja baada ya vijana hao kupata elimu walijitoa kwenye vitu hivyo
.
.
 Kwa hiyo vitu kama hivi vya kijamii vidogo vidogo ndio kimewavutia Umoja wa nchi za Ulaya na kuona wanastahiki kumpa Fid  tuzo hiyo“alisema.

No comments:

Post a Comment

advertise here