Wednesday, 3 May 2017
Monday, 1 May 2017
TUNDU LISSU AKOMALIA VYETI VYA BASHITE KOTINI
WAWKILI Tundu Lissu na wenzake wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelikomalia vilivyo sakata maarufu la Bashite linalohusiana na tuhuma za kughushi vyeti vya kielimu linalomkabili mmoja wa wakuu wa mikoa kwa kulifikisha kortini ili lipatiwe ufumbuzi.
Aidha, Lissu na wenzake hao wamedhamiria kuona kuwa kigogo huyo anayetuhumiwa kuliacha jina lake halisi la Daudi Albert Bashite kutokana na matokeo mabovu ya sekondari na kutumia jina la mtu mwingine, achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela kwa kosa la kughushi ikiwa itathibitika kuwa ana hatia.
Sunday, 30 April 2017
Saturday, 29 April 2017
FREEMASON: HUU NDIO UTAJIRI ALIOUACHA KIONGOZI WA FREEMASON SIR CHANDE
MTANDAO maarufu wa Wikipedia umedai kwamba hayati Jayantilal Keshavji Chande (Sir Andy Chande) ameacha utajiri wa kiasi cha dola milioni 892; unaomfanya kuwa na utajiri mkubwa kuliko ule wa Said Bakhresa, ingawa watu waliokuwa karibu naye wanakana kuwa na utajiri wa aina hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao huo, Bakhresa ana utajiri wa thamani ya dola milioni 560 (shilingi trioni 1.2) akiwa nyuma ya Mohamed Dewji aliyetajwa na jarida la Forbes kuwa na utajiri wa dola bilioni 1.1
Friday, 28 April 2017
Thursday, 27 April 2017
TRA YAKAMATA MALI ZA LUGUMI

Kampuni ya udalali ya Yono, imefanikiwa kukamata mali za wafanyabiashara wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya kukamata mali hizo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam imefanywa ndani ya wiki moja.
Wednesday, 26 April 2017
HAYA NDIO MADHARA 12 YA KUJICHUBUA NGOZI
Tabia ya kujichubua ilianza kupata umaarufu kwanzia mika ya 1980 mpaka miaka ya hivi karibuni, hii hasa kwenye nchi za watu ambao hawana ngozi nyeupe kabisa kama waarabu, wahindi na waafrika. biashara hii imewafanya watu wanaotengeneza bidhaa hizi kua matajiri sana huku zikiacha madhara makubwa kwa watumiaji.
Monday, 24 April 2017
Sunday, 16 April 2017
MIILI YA ASKARI POLISI 8 WALIOUAWA PWANI YAAGWA...WAZIRI ATANGAZA KIAMA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewatangazia kiama watu wote waliohusika kuwaua askari polisi nane Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam jana asubuhi Mwigulu alisema watu hao watakamatwa wote na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
"Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata"alisema Mwigulu.
Friday, 14 April 2017
CUF YA LIPUMBA YAAPA KUMCHANACHANA MAALIM SEIF..!!!
KURUGENZI ya Ulinzi ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof Ibrahim Lipumba
Imedai itazuia ziara za Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ambazo amepanga kufanya Dar es Salaam, ikiwa hataishirikisha kurugenzi hiyo kwa ajili ya ulinzi.
Wednesday, 12 April 2017
VIDEO: WAZIRI MWAKYEMBE AJIBU KWANINI ALIHUDHURIA ‘PRESS’ YA ROMA

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni, na Michezo, Prof. Harrison Mwakyembe amesema kuwa anamshangaa Mbunge wa Jimbo la Chemba Mkoani Dodoma, Juma Nkamia kuhoji uwepo wake katika mkutano wa mwanamuziki wa bongofleva ‘Roma’ na waandishi wa habari uliofanyika juzi Jijini Dar es salaam.
Video: MBUNGE WA NKASI ACHEKELEA ROMA KUPEWA KIBANO...ATAKA WASANII WANAOMTUKANA RAIS WAPEWE KIBANO ZAIDI

Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Keissy amefunguka na kusema wasanii ambao wanaandika nyimbo za kumtukana na kumkashfu Rais Magufuli wanapaswa kupata kibano zaidi ili waache tabia hiyo
Mbunge huyo amesema hayo leo bungeni na kusema angeaachiwa yeye dakika mbili tu wangeona ni nini angewafanya, hivyo kuendelea kuwatetea wasanii hao ni jambo ambalo si sawa, na kusema wasanii hao wajaribu kwenda Rwanda au nchi za kiarabu waone jinsi watakavyonyongwa.
ILE KESI YA GWAJIMA YA KUMTUKANA ASKOFU PENGO..LEO JAJI AMECHUKUA MAAMUZI HAYA MAZITO..!!!
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya kutoa lugha chafu inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha aliifuta kesi hiyo leo chini ya kifungu cha 225 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA).
Kesi hiyo imefutwa baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Maugo kueleza kuwa hawakuwa na shaidi na kuomba wapewe ahirisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)