Akiwa ni
miongoni mwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji
Joseph Warioba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema
msimamo wake bado upo kwenye Rasimu ya Katiba hiyo.
Polepole
aliipigia debe la nguvu rasimu hiyo ambayo miongoni mwa mapendekezo yake ni
uwapo wa Serikali tatu; Shirikisho, Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza
kwenye ofisi za gazeti hili wiki hii jijini Dar es Salaam, Polepole alisema
msimamo wake bado uko kwenye Rasimu ya Jaji Warioba.
“Msimamo
wangu ndivyo ulivyo muda wote tangu mwanzo hata sasa na CCM inaamini hivyo,
kuheshimu maoni ya wananchi,” alisema Polepole na kuongeza:
“Hatuwezi
kupuuza watu kwa namna yoyote, CCM haiko hapa kupuuza watu bali kuwasikiliza na
ndiyo maana msingi wa mageuzi ya chama ni kuwa cha wanachama, unapokuwa na
chama cha wanachama unakuwa daraja kati ya wananchi na Serikali.”
Kuhusu
utawala wa Rais John Magufuli kwa suala la Katiba, alisema kumekuwa na mageuzi
yanayofanywa kabla ya kufikia kwenye mchakato wa Katiba.
Credit -
Mwananchi
No comments:
Post a Comment