Sunday, 30 April 2017

ZITTO KABWE: KUHUSU NDEGE MPYA BOEING AFUNGUKA MAKUBWA



Sakala la Serikali kusemekana imenunua ndege ya Boeing ambayo ina walakini imechukua sura mpya baada ya Mbunge Zitto Kufunguka Haya Hapa chini kupitia page yake ya Facebook:

"Hizi Ndio Habari za kina kuhusu ndege ya Boeing 787 Dreamliner tuliyokwishalipia. Ni sehemu ya ndege zilizokuwa chini ya kiwango zikiitwa Terrible Teens. Iliundwa mwaka 2009 na kununuliwa na ReandAir Tarehe 21/11/2013. Baada ya Mwaka, tarehe 3/12/2014, Rwanda wakaikataa na kuirudisha. Tanzania imeinunua tarehe 14/12/2016 Kwa dola za kimarekani 224 milioni. 
Sasa, mwanzo nilitaka maelezo ya Serikali, wasemaji wa Serikali wakawa wengi Sana kuwa tuliyonunua sisi sio terrible tween. Nimefanya utafiti kidogo na NIMETHIBITISHA kuwa tumenunua ndege zilizokatawaliwa hata na Rwanda rafiki zetu. Kinachofuata ni kikubwa zaidi. Watetezi wa Serikali muwe tayari kuja kutetea pia maana labda mna mgawo. Kifuatacho NCHI ITATIKISIKA" Zitto Kabwe



No comments:

Post a Comment

advertise here