Tuesday, 22 November 2016

U HEARD: MAJIBU YA DIAMOND JUU YA MWANAYE “TIFFA” KUOLEWA NA MTOTO WA ALIKIBA

Kutoka ndani ya XXL leo November 22, 2016 U Heard imekuja na stori kuhusu picha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha watoto wa mastaa wa Bongo Flava, Diamond Platnumz na Alikiba huku ikiwa imeandikwa (Natamani mkikua mje kuoana ili baba zenu wapatane).
Kwa mujibu wa Soudy Brown baada ya kuzagaa kwa picha hiyo, kuna tajiri fulani jijini Dar es
salaam ambaye inadaiwa ni shabiki wa wasanii hao, amejitokeza na kusema yuko tayari kumlipia mahari mtoto wa Alikiba ili aje kumuoa Tiffa, mtoto wa Diamond.
Soudy Brown amezungumza na Diamond Platnumz kuhusu suala hilo na je ana maamuzi gani juu ya mwanaye kutolewa mahari.
“Ntampiga hela zake hatokaa aamini, sijajua ntataka walipe kiasi ila sitatoa bure uislamu huo sina mimi, eti sijui uje tu na kitabu aaah wapi, hapa hela tu tena itakua hela nyingi sana labda itokee mwenyewe atunuku ila kama atanisikiliza mimi baba yake atapiga hela nyingi  tu hata Dola milioni 1 ndogo” – Diamond

No comments:

Post a Comment

advertise here