Sunday, 27 November 2016

LIVERPOOL YAPATA PIGO

 Philippe Coutinho amepata majeraha mabaya wakati wa kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Liverpool dhidi ya Sunderland.

Uwanja wa Anfield ulizizima kwa ukimya wakati fundi huyo wa kibrazil akiwa chini huku wakiwa na shauku ya kutaka kujua itachukua muda gani nyota wao kurejea tena kwenye pitch.



Coutinho amekuwa kwenye ubora wake msimu huu huku ndoto za ubingwa zikiwekwa mabegani mwake.

Licha ya kwamba Liverpool si timu inayotegemea mchezaji mmoja, lakini bila shaka Coutinho amekuwa mtu muhimu wakati timu ikishambulia kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza nafasi pamoja na kufunga magoli.

Hadi sasa bado ukubwa wa tatizo haujafahamika lakini kwa muonekano wa picha, inaonekana tatizo ni kubwa na huenda Klopp akosa huma ya raia huyo wa Brazil kwa muda mrefu.
Kuna uwezekano akawa alivunjika mguu wakati akigombea mpira na mlinzi wa Sunderland Didier Ndong.

No comments:

Post a Comment

advertise here