Friday, 26 August 2016

JE? UNAJUA SABABU YA KUHARIBIKA KWA MIMBA


Tatizo la mimba kutoka au kutolewa ni jambo ambalo limewakumba kina mama wengi walio katika umri wa kuzaa. Aidha mijadala kuhusu kuhalalishwa au kuendelea
kuharamishwa kwa utoaji mimba ni jambo linalochukua nafasi ya mazungumzo ya kila siku katika maisha yetu.

Kwa baadhi ya nchi, suala la utoaji mimba ni jambo lililohalallshwa kisheria ingawa kwa nchi kama Tanzania, suala hili halijahalalishwa isipokuwa tu pale panapokuwa na sababu za kitabibu zinazolazimisha kufanya hivyo.



Nini maana ya mimba kutoka (abortion)

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), utokaji mimba (abortion) hutokea pale ambapo kiumbe (mimba) kilicho chini ya wiki 22 kinapotoka kwa sababu moja ama nyingine, au kinapotolewa kwa njia yeyote ile. Aidha shirika la Afya limekwenda mbali zaidi na kutoa maana nyingine ya utokaji mimba kuwa ni pale mtoto (kiumbe) anapozaliwa akiwa na uzito wa chini ya gram 500.

Aidha baadhi ya matabibu hupendelea kutumia neno 'abortion' kumaanisha kitendo cha utoaji wa mimba kinachofanywa na mtu mwingine ama kwa njia sahihi au zisizo sahihi na 'miscarriage' kumaanisha kitendo cha mimba kutoka yenyewe kwa sababu nyingine yeyote. Ukiacha tofauti hizi za jinsi ya kuharibika kwa mimba, abortion na VIDEO COMMERCIAL DEMO miscarriage humanisha kitu kilekile cha mimba kutoka.

Aina za utokaji/utoaji mimba (Classification of abortion)

Utokaji mimba umeanishwa katika aina zifuatazo

1. Utokaji wa mimba wa hiyari yaani kitendo cha mimba kutoka yenyewe (spontaneous abortion)

2. Mimba inayotishia kutoka ingawa bado haijatoka (threatened abortion)

3. Utokaji wa mimba usioepukika (inevitable abortion)

4. Utokaji wa mimba ulio kamili (complete abortion)

5. Utokaji wa mimba usio kamili (incomplete abortion)

6. Mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)

7. Utokaji wa mimba unaojirudia rudia (recurrent abortion)

8. Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)

9. Utoaji mimba kwa sababu za kiafya (therapeutic abortion)

Utokaji mimba kwa hiari au kitendo cha mimba kutoka yenyewe (spontaneous abortion)

Hii ni hali inayotokea pale mimba inapoharibika na kutoka bila kuwepo kwa sababu yeyote iliyo dhahiri, kwa maana nyingine mimba uharibika na kujitokea bila kusababishwa na mtu wala kitu chochote.

Utokaji mimba wa namna hii umegawanyika katika aina kuu nne ambazo ni

1. Mimba inayotishia kutoka ingawa bado haijatoka (threatened abortion)

2. Mimba isiyoepukika kutoka (Inevitable abortion)

3. Mimba inayotoka yote au kamili (complete abortion), na

4. Utokaji mimba usio kamili (Incomplete abortion)

Mimba inayotishia kutoka (threatened Abortion)

Tatizo hili hutokea mapema wakati wa ujauzito. Hali hii hujionesha kwa damu kutoka ukeni wakati njia ya shingo ya uzazi ikiwa bado imefunga. Mara nyingi mimba inayotishia kutoka haina tabia ya kuambatana na maumivu yeyote ya tumbo.

Daktari anapompima mgonjwa hukuta shingo ya kizazi ikiwa imefunga na hakuna dalili zozote za kiumbe kutoka ingawa mgonjwa hutokwa na damu sehemu za siri. Aidha mgonjwa huwa hana maumivu yeyote ya tumbo.
nakala hii imeandaliwa na dr mandai MANDAI HERBALIST CLINIC 0716 300 200

No comments:

Post a Comment

advertise here