Thursday, 7 July 2016

YOUNG D:NIMEMRUDIA MUNGU SASA

subscribe katika channel yetu hapa
Msanii Young D ambaye siku za karibuni ameweza kuachana na matumizi ya dawa za kulevya amefunguka na kusema kwa sasa ameamua kumrudia Mungu ili kujijenga na kuzidi kujiimarisha zaidi kiimani ili asiweze kurudi gizani alikotoka.
YOUNG D
Young D
Young D amesema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Young D anadai kuwa alikuwa anapigana vita kati ya nafsi na roho kwa yeye kushinda vita hiyo imempa nafasi kuweza kutumia muda wake wa ziada kusoma sana biblia na vitabu vya dini ili kujiimarisha kiimani ili asiweze
kuteteleka na mambo ya dunia.
“Unajua kila jambo na changamoto zake, mimi nilikuwa napigana vita kati ya nafsi na roho, na nimeweza kushinda vita hiyo saizi siitaji mwili wangu uniendeshe mimi bali mimi nasikiliza moyo wangu zaidi, na kiukweli toka nimeacha haya mambo saizi naona mwanga katika maisha yangu. Kwa sasa napokuwa nipo huru sina kitu cha kufanya natumia muda huo kusoma sana vitabu vya Mungu ili kujiimarisha kiimani, huwezi kuamini saizi ukichukua simu yangu utakutana na ‘Appilication’ ya Biblia ya Kiswahili kwani ndiyo vitu vinaweza kunijenga imani ili nisiweze kurudi gizani nilikotoka” alisema Young D
Mbali na hilo Young D alisema kuwa katika kipindi ambacho alikuwa gizani mtu ambaye alikuwa anaumia zaidi ni mama yake mzazi pamoja na mashabiki zake lakini kwa sasa anafuraha sababu yeye mwenyewe anaona mwanga na jinsi watanzania walivyoweza kumsamehe na kumpokea vizuri.
“Unajua mama yangu mzazi ananipenda sana, alikuwa anasikia mambo kutoka kwa watu na mimi nilikuwa nikifika naweza labda kumuachia pesa lakini nikagundua vyote navyofanya havina thamani kwake kama nitaendelea na maisha yangu yale, kiukweli alikuwa anashindwa kusema lakini alikuwa anaumia sana moyoni mwake” aliongeza Young D

No comments:

Post a Comment

advertise here