Saturday, 25 June 2016

OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI KUHAKIKI VYAMA KUANZIA TAREHE 27 JUNI HADI TAREHE 06 JULAI, 2016

subscribe hapa 
Jaji Francis S.K. Mutungi
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini inapenda kuwafahamisha wananchi kwamba, kuanzia tarehe 27 Juni, 2016 hadi tarehe 06 Julai, 2016 itaendesha zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa mengine ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1992, kwa Vyama vya Siasa vyenye usajilli wa kudumu kwa upande wa Tanzania Bara.


Zoezi hili ni endelevu kwani ni utekelezaji wa kawaida wa majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Hufanyika kila mwaka isipokuwa kwa mwaka jana (2015) kwa kuwa ulikuwa mwaka wa uchaguzi.
Zoezi la uhakiki kwa upande wa Zanzibar litafanyika baada ya zoezi kukamilika Tanzania Bara kwa tarehe ambazo zitatangazwa baadaye.
Ofisi inatoa rai kwa vyama vyote vyenye usajili wa kudumu kulipa kipaumbele zoezi hili, kwani ni zoezi ambalo linagusa uhai wa kila chama.
Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
24 JUNI, 2016

KAMA ULIKOSA KUSKIA HOTUBA FUPI YA ZITTO KABWE ICHEKI HAPA MTU WANGU

No comments:

Post a Comment

advertise here