LAYIII
BONYEZA PICHA KUJIUNGA NA MTOTO HAPPY
BONYEZA PICHA KUJIUNGA NA MTOTO HAPPY
Mahakama ya katiba Korea kusini imeendelea kukataa rufaa
iliyowasilishwa kupinga sheria inayopiga marufuku biashara ya ngono
ikiwa ni ishara ya kushindwa kwa wafanyabiashara hii ambao kwa miaka
mingi wamekuwa wakifanya kampeni kupinga hayo maamuzi.
Hakimu Kim chang jong amesema kampeni za kuleta uwazi na
uhuru katika ngono hazimaanishi kuwa
biashara inayohusisha ngono ni kitu
halali, sheria ambayo ilipitishwa mwaka 2004 inasema watu wanaofanya
biashara ya kujiuza na wateja wao watahukumiwa kulipa faini au kutumikia
kifungo cha hadi mwaka mmoja gerezani endapo watakutwa na hatia ya
kujihusisha na biashara hii.
Haya maamuzi yaliungwa mkono na majaji wengine watano
kwenye mahakama ya katiba ya korea ya kusini ambapo hata hivyo upinzani
mkubwa kwa sheria hii ulionekana toka kwa majaji wengine watatu ambapo
mmoja alipinga kuharamishwa kwa biashara ya ngono akisema kuwa sheria
hiyo inaathiri mustakabali wa baadhi ya wanawake ambao hutegemea
biashara hii kuendesha maisha yao.
Majaji waliounga mkono kuhalalishwa kwa biashara hii
wamesema kuwa si kweli kwamba biashara ya ngono inashusha utu au hadhi
ya ubinadamu kwani tishio la ustawi wa uhai wa mtu pale anapokosa
shughuli ya kuendesha maisha yake ndio kitu kinachoshusha utu wa
mwanamke zaidi ya biashara ya ngono.
Mwaka jana Mahakama hii ya katiba ilifanya maamuzi ya
kihistoria wakati ilipopitisha sheria ya kuhukumu kosa la zinaa kwa
kifungo cha miaka miwili yakiwa maamuzi yaliyoakisi mtazamo hasi wa
jamii ya korea ya kusini katika masuala ya kijamii ikiwemo ngono.
No comments:
Post a Comment