Bunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng'oa rais Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne.
Spika
wa bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo baada ya shinikizo
kutoka kwa vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Economic Freedom
Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema.
Spika Baleka
Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais
Zuma kufuatia tuhuma za ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi
mabaya ya madaraka yake.
Vyama vya upinzani vilikuwa vimemtaka ajiuzulu baada ya kupatikana na
hatia ya kutumia madaraka yake vibaya kwa kuidhinisha ukarabati wa
makazi yake licha ya kushauriwa asifanye hivyo.
Siku ya Alhamisi,
mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa rais amekwenda kinyume na katiba,
katika kashfa ya mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kukarabati nyumba yake
ya binafsi.
Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana
Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati
wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.
Mahakama ilisema wizara ya fedha itatambua ni kiasi gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma atatakikana kuzirejesha.
Rais Jacob Zuma alikubali uamuzi wa mahakama ya kikatiba uliompata na
hatia na akaapa kulipia ukarabati uliofanyiwa makao hayo ya Nkandla
kama ilivyoamua mahakama.
No comments:
Post a Comment