Sunday 3 April 2016

HUYU NDIYE MSANII WA KIUME AMBAYE LADY JAYDEE ANAMFIKILIA KWA SASA

LAYIII
NJOO YOUTUBE BONYEZA PICHA HII KUJIUNGA NAMI YOUTUBE
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Ndi ndi ndi' amefunguka na kuweka wazi wazi msanii wa kiume ambaye kwa sasa anamfikiria katika kufanya nae kazi.

Kupitia Accout yake ya twitter ambapo alitoa nafasi ya maswali kutoka kwa mashabiki zake Lady Jaydee aliulizwa swali kama ataweza kufanya remix ya wimbo wake mpya na kama

atafanya hivyo anadhani ni msanii gani wa kiume ambaye ataweza kufanya nae kazi hiyo. Ndipo hapo aliposema kwa sasa anamfikiri sana Mr Blue.

"Kiukweli mtu niliemfikiria hapo ni Mr Blue, naona ndio ata fit vizuri zaidi, Msanii wa Tanzania alieko akilini kwangu hivi sasa ni Mr Blue" alisisitiza Lady Jaydee.

Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi sababu za ukimya wake kwenye muziki kabla ya kuja na wimbo huo mpya na kusema kuwa huo ndio utaratibu wake toka amenza muziki na toka anatoka na Album ya kwanza mwaka 2001 yeye si mtu ambaye anatoka ngoma mara kwa mara bali huwa anajipa muda ya kujiandaa lakini hata hivyo nyimbo anazokuwa anatoa zinadumu muda mrefu ndiyo maana anakosa sababu ya kuharakisha kutoa kazi kila siku.

"Ndio utaratibu niliojiwekea miaka yote tangu Album ya kwanza 2001, mimi huwa sio msanii wa back to back lakini uzuri nyimbo zenyewe hudumu miaka mingi hivyo nakosa sababu ya kuharakisha kutoa kazi kila siku. Zitakapoisha nyimbo zilizomo kwenye album hii ya 7 itachukua muda tena kutoa zingine. Huwa najiandaa" alisema Lady Jaydee.

Baadhi ya mashabiki walitaka kufahamu msimamo wake juu ya wasanii kutumia vilevi na madawa ya kulevya na ndipo hapo Lady Jaydee aliposema kuwa ni sawa kutumia dawa za kulevya ila hyaina ubaya kwa msanii au mtu kutumia kilevi kidogo na kusema ili mradi usiwe kero kwa watu wengine.

"Si sawa kutumia dawa za kulevya ila haina ubaya kujichangamsha na Lager kiasi ilimradi usikere watu wengine. Vilevi vinatofautiana vipo visivyofaa vyenye madhara, si halali, situmii. Natumia halali Kama Wine na Beer". Lady Jaydee.



No comments:

Post a Comment

advertise here