LAYIII
Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa uchaguzi huo kuahirishwa baada ya tume
ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi kwa majuma matatu kutokea tarehe 26 Juni
hadi tarehe 15 Julai
Burundi:Uchaguzi waahirishwa tena
Uchaguzi wa Burundi umeahirishwa tena.
Msemaji wa Rais Pierre Nkurunziza amesema uchaguzi utafanyika tarehe 21 Julai.
Uchaguzi
huo umekumbwa na utata baada ya makundi ya upinzani kuandamana na
kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Upinzani unadai kuwa rais Nkurunziza anakiuka katiba ya taifa na mapatano ya Arusha yaliyokomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa
mujibu wa Msemaji wa rais ,Gervais Abayeho uchaguzi huo umeahirishwa
kutoka tarehe 15 hadi tarehe 21 kufuatia shinikizo la viongozi wa kanda
ya Afrika mashariki na Kati.
Viongozi hao wakiwemo mwenyekiti na
mwenyeji wa jumuiya, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Yoweri Museveni
wa Uganda, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta waliendekeza uchaguzi
uahirishwe kufuatia mgogoro wa kisiasanchini Burundi.
Shinikizo lilitokana na Umoja wa Afrika, na Umoja wa mataifa, jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki
Zaidi ya raia laki moja wa Burundi wamekimbia nchi hiyo tangu mwezi
Aprili wakati kulizuka ghasia kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza
kuwania muhula wa tatu.
Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa uchaguzi
huo kuahirishwa baada ya tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi kwa majuma
matatu kutokea tarehe 26 Juni hadi tarehe 15 Julai
No comments:
Post a Comment