Tuesday, 23 June 2015

Fid Q aja na kampeni ya ‘TUVISHANE’, wasanii wa Arusha waungana kusaka vipaji, Je ni kweli Ali Kiba ana bifu?…#255 (Audio)

layiii
Leo Perfect Crispin kapiga stori na Farid Kubanda, ameanzisha kampeni ya TUVISHANE, ikiwalenga wale wote ambao hununua nguo nzuri na kujikuta hawazivai kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kudai zimepitwa na

kiba
Leo Perfect Crispin kapiga stori na Farid Kubanda, ameanzisha kampeni ya TUVISHANE, ikiwalenga wale wote ambao hununua nguo nzuri na kujikuta hawazivai kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kudai zimepitwa na wakati na yeye kuona umuhimu wa kuanzisha kampeni ya kuomba watu kujitokeza kuwapa nguo wale watu ambao hawana uwezo ili ziweze kuwasaidiaameona awaombe watu kujitokeza kuwasaidia watu ambao wameona hawavai.
Pia amezungumza na wasanii wa Arusha ambao wameamua kuungana na kuleta maendeleao kuhusu muziki wetu, ambapo Chindo Man ambaye ni mmoja wa wasanii kutoka Mkoani humo pamoja na wasanii wenzake wameanzisha project kwa ajili ya kukusanya vijana ambao wapo mitaani ili kuwapa elimu na kisha kupewa vyeti ili kupata wanamuziki bora wa baadaye kuliko kukaa mitaani bila kazi yoyote.
Ali Kiba naye ameamua kuanzisha tour ya ndani kwa washkaji zake ambao wanatumia usafiri wa daladala ambapo ameamua kufanya hivyo baada ya mashabiki wake kumuona ni mtu wa watu, na atakua akitumia usafiri huo katika Wilaya zote za Dar es salaam ili kupiga nao stori kwa kuwa anamini kuna watu wanatamani kuzungumza naye lakini hawapati nafasi hiyo.
Pia amesema yeye na Diamond huwa hawashirikiani, lakini kwa upande wa timu zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii hawezi kuwazuia kwa sababu hana nguvu hiyo kwa sababu hawajui ni kina nani.
Zote zisikilize hapa…


No comments:

Post a Comment

advertise here