LAYIII
Msanii na mmoja kati ya watu wanaounda team ya Cash Money Records Lil Wayne aliingia kwenye headlines kipindi cha nyuma
Msanii na mmoja kati ya watu wanaounda team ya Cash Money Records Lil Wayne aliingia kwenye headlines kipindi cha nyuma
Drake na Nicki Minaj kuondoka Cash Money Records!? Stori nzima ipo hapa.
Msanii na mmoja kati ya watu wanaounda team ya Cash Money Records Lil Wayne
aliingia kwenye headlines kipindi cha nyuma kwa madai ya kutaka kutoka
katika label hio ya muziki.
Headlines mpya leo ni kwamba msanii huyo wa Hiphop amefungua kesi mahakamani dhidi ya Cash Money kwa madai ya kwamba eti Nicki Minaj na Drake hawana usimamizi mzuri chini ya lebo hio.
So ina maanisha Nicki Minaj na Drake wako njiani kuimwaga Cash Money Records? ama ni stori tu!?
Katika documents zilizowasilishwa mahakamani Lil Wayne amedai
kua sio yeye peke yake anae wadai lebo ya hio ya muziki bali lebo hio
imeendelea kukataa kuwalipa wasanii wengine chini ya lebo hio pesa zao,
na kusisitiza kua visa hivi vitasababisha yeye na baadhi ya wasanii
aliowaleta kwenye lebo hio kutemana na Cash Money Records.
Msaani huyu alieibua vipaji vya Drake, Nicki Minaj na J.Prince amedai kua Birdman alimuahidi asilimia kubwa ya pesa ya Cash Money Records kutoka kwenye faida ya kumgundua Drake alieiingizia lebo hio faida zaidi ya dola millioni 40 lakini akashangaa jamaa amemlipa millioni mbili tu kati ya mamilioni aliotakiwa kulipwa.
No comments:
Post a Comment