Arsenal imeambulia alama moja nyumbani kwa Bournemouth baada ya kutoka nyuma kwa magoli 3-0.
Ilikuwa
nii kama kutimiza lengo kwa the Gunners baada ya kufunga magoli matatu
ndani ya dakika 20, kabla ya hapo Bournemouth ambao walikuwa wenyeji
walikuwa wakiongoza kwa magoli 3-0.Alexis Sanches alianza kuiandikia bao la kwanza Arsenal dakika ya 70 kabla ya Lucas Perez
kuandika bao la pili dakika tano baadae.
Bournemouth ilianza kuyumba baada ya nahodha wake Simon Francis kulimwa kadi nyekundu dakika ya 83 na kuachia mwaya kwa Arsenal kuutawala zaidi mchezo ambapo dakika ya 90 Olivier Giroud aliisawazishia timu yake na kupelekea kugawana alama moja moja.
Kwa matokeo hayo Arsenal wanasalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama 42 huku AFC Bournemouth wakipanda mpaka nafasi ya tisa wakiwa na alama 25 kibindoni.
No comments:
Post a Comment