BONYEZA PICHA HAPA KUJIUNGA NAMI YOUTUBE USIACHE KUSUBSCRIBE MTU WANGU
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA) imetangaza bei mpya za Petrol, Diesel na mafuta ya Taa zinazoanza kutumika leo Jumatano huku bei ya mafuta ya Taa na Diesel ikiwa imeshuka kwa wastani wa shilingi 66 kwa lita.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix Ngamlagosi inaonesha
kuwa kwa wastani kumekuwa na ongezeko dogo sana la bei ya mafuta ya
Petroli ambayo kwa jiji la Dar es Salaam bado itauzwa kwa bei ile ile
ilivyokuwa mwezi wa 12, 2016.
IJUWE MIJI KUMI MICHAFU ZAIDI DUNIANI MTU WANGU
IJUWE MIJI KUMI MICHAFU ZAIDI DUNIANI MTU WANGU
Hata
hivyo, taarifa hiyo imetoa ruhusa kwa wauzaji wa jumla na rejareja wa
mafuta nchini kuuza bidhaa hiyo kwa bei ndogo zaidi chini ya bei elekezi
iliyotangazwa na mamlaka hiyo ikiwa ni njia ya kuongeza ushindani kati
ya wauzaji wa nishati hiyo nchini.
No comments:
Post a Comment