Wednesday, 16 November 2016

DONALD TRUMP AZIKATAA DOLA 400,000 ZA MSHAHARA WA RAIS..ADAI ATAJILIPA DOLA 1 KWA MWAKA

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema hataki kulipwa mshahara wa rais wa $400,000 atakapochukua hatamu Januari mwakani. Badala yake atakuwa akilipwa dola moja ya Marekani ($1) pekee kila mwaka  sawa na shilingi 2000 ya kitanzania.



Alifichua mpango wake huo wakati wa mahojiano na Lesley Stahl kipindi cha 60 Minutes cha CBS News.

Ingawa hakujua rais huwa analipwa pesa ngapi, Bw Trump alisema alidhani anahitaji kuchukua tu $1.

Baada ya Bi Stahl kumjulisha kwamba mshahara wa rais ni $400,000, alisema: "Hapana, sitaupokea mshahara huo. Sizichukui kamwe."

Rais huyo mteule anatimiza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni.

Aliambia waliohudhura mkutano wake Septemba kwamba mshahara wa rais si jambo kubwa kwake.

No comments:

Post a Comment

advertise here