like page yetu facebook hapa SWAXBZ ili usipitwe na kila story inayotufikia
Karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri ambapo tunajadili changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha.
Leo tutajadili changamoto ya ukosekanaji wa mitaji na jinsi ya kuipata. Kabla hatujaanza kujadili changamoto hii naomba niweke maoni ya wasomaji waliotuandikia kuhusu hili;
Mimi ni graduate wa diploma ya uhandisi magari, kila nikifikiria kuanza kuijajiri nashindwa kutokana na kipato cha kuanzia biashara.. je nifanyeje niweze kupata kipato cha kujiajiri?
Napenda sana kufanya biashara ila tatizo ni eneo la kufanyia, ama kodi nikubwa sana na maeneo hakuna Changamoto Ni Kutokuwa Na Mitaji Ya Kukusaidia Kupanua Biashara, Hata Kama Ukipata Fursa, Swala Linabakia Mitaji Nimtaji, Kwani Ubunifu Unaendana Na Fedha Ya Kuanzia.
Namna ya kupata mtaji. Biashara niiwazayo ni Duka la vifaa vya ujenzi na Umeme. Kodi ya eneo husika ni kama efu 60 kwa mwezi!!
Ukosefu wa mtaji na sijui nitumie njia gani kupata.Hayo hapo juu ni baadhi ya maoni ya wasomaji wenzetu kuhusiana na changamoto ya mtaji.
Kikwazo kikubwa cha kuanza au kukuza biashara sio mtaji.Ndio nasema kwamba tatizo linalokuzuia wewe kuanza au kukuza biashara sio mtaji bali ni wewe mwenyewe.
Mtaji umekuwa ukitumika kama sababu ya watu kutokuumiza vichwa ili kujua wanawezaje kuingia kwneye biashara. Kila mtu utakayeongea nae kuhusu biashara ataanza na tatizo ni mtaji.
Ukimuuliza ni mtaji kiasi gani anahitaji anaweza kukujibu, ukimuuliza utautumiaje, hana mpango huo, ukimuuliza kama hutapata kiasi chote hicho unachotaka unaweza kuanzia kiasi gani halafu ukaendelea kukua pia hatakuwa na majibu.
Hii ndio inanisababisha niamini kwamba kikwazo cha kwanza sio mtaji bali mtu mwenyewe.
Wakati nafikiria njia za kupata mtaji wa kuanzia biashara miaka mitatu iliyopita, niliamua kuchukua kazi ambayo haikuwa na malipo makubwa. Wafanyakazi niliowakuta pale kila tulipokuwa tunazungumzia biashara walikuwa wakilalamikia mtaji.
Nilifanya kazi pale kwa mwaka mmoja, nikapata mtaji wa kuanzia biashara, lakini mpaka leo nikikutana na wafanyakazi wale wanasema tatizo ni mtaji. Sasa hebu niambie kama unasema tatizo ni mtaji kwa zaidi ya miaka miwili bado unaendelea kuamini tatizo ni mtaji kweli? Hapana, tatizo ni wewe mwenyewe.
Kuna njia nyingi sana za kutatua tatizo lako hilo la kushindwa kupata mtaji. Hapa nitazungumzia tano unazoweza kuanza kufanya leo na siku zijazo ukasahau kabisa kuhusu tatizo hilo.
1. Tumia akiba zako, au anza kuweka akiba.
Kama kuna akiba zozote ambazo umekuwa unajiwekea kwa muda unaweza kuzitumia kwa kuanzia biashara. Kama huna akiba yoyote anza sasa kujiwekea akiba na jipe muda unaohitaji ili kufikisha kiwango cha mtaji unachotaka.
Kama unaona kipato unachopata huwezi kuweka akiba tumia njia hii rahisi ya kuweza kuweka akiba (bonyeza maandishi yaliyokolezewa wino kusoma zaidi).
2. Chukua kazi hata yenye maslahi kidogo.
Kama ndio umemaliza shule na hujapata ajira na pia huna mshahara wa kuanzia nakushauri uchukue kazi yoyote unayoweza kupata hata kama ina maslahi kidogo.
Lengo lako litakuwa ni kukusanya mtaji na hivyo utaifanya kazi hiyo kwa kipindi fulani na kisha kuachana nayo.
Inabidi ukubali kuteseka kwa muda kidogo ili uweze kufika kule unakotazamia. Sasa kama utaniambia kwamba wewe ni msomi na kuna kazi huwezi kufanya, nitakuambia uendelee kuimba tatizo ni mtaji.
3. Anza kidogo.
Unapoanza biashara hasa pale unapoanzia sifuri ni vigumu sana kuweza kupata kiasi chote cha fedha unachohitaji. Unaweza kuanza kidogo na baadae ukaendelea kukua na pia kujifunza.
Jua ni kiasi gani unahitaji kama mtaji na gawa kwenye kiasi kidogo ambacho unaweza kuanzia. Ukisema usubiri mpaka upate kiasi kikubwa unachofikiria itakuchukua muda mrefu sana na baadae utakata tamaa. Kama unafikiri haiwezekani, Soma; Safari ya mafanikio ya John (kutoka milioni 4 mpaka milioni 100).
4. Ungana na mwenzako mwenye mawazo kama yako.
Unaweza kuungana na mwenzako au wenzako wenye mawazo kama yako na mkaunganisha fedha kidogo mlizo nazo na kuweza kuanza biashara. Hii ni njia nzuri sana ya kuweza kuunganisha mitaji kidogo ambayo unaweza kuitumia na ukafikia mafanikio makubwa.
Ila ni muhimu sana kuwajua vizuri wale unaoshirikiana nao kabla hamjaingia kwenye ushirikiano kwa sababu wanaweza kuwa kikwazo cha wewe kufikia mafanikio unayotarajia. Nilianza bishara ya kwanza kwa njia hii na hata sasa biashara tatu kati ya nne ninazofanya ninashirikiana na watu wengine.
5. Anza na biashara ambayo haihitaji mtaji.
Sasa hivi tunaishi kwenye ulimwengu ambao kila mtu, yaani kila mtu anaweza kuwa tajiri mkubwa bila ya kujenga kiwanda(kama ilivyokuwa zamani).
Mtandao wa intaneti umeleta mapinduzi makubwa sana kwenye maendeleo. Unaweza kuanza kufanya kazi na ikakuingizia kipato bila ya kuwa hata na ofisi.
Nilianza biashara ya kwenye mtandao wa intanet bila ya kuweka gharama yoyote zaidi ya kompyuta yangu na intanet ambayo naipata kwenye malipo mengine ya simu na sasa ina mafanikio makubwa sana.
Ukiacha biashara za kwenye mtandao wa intaneti kuna biashara za mtandao(Network Marketing) ambapo unaweza kuanza biashara hizi kwa mtaji kidogo na ukakua sana kwa juhudi utakazoweka.
Kupata maelezo zaidi kuhusu biashara hizi soma; barua ya wazi kwa wahitimu ambao bado wanazungusha bahasha.
6. Nyongeza, Uza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa navyo.
Hapa nakwenda moja kwa moja kwa vijana hasa waliomaliza masomo karibuni. Kama unataka kuanza biashara ila huna mtaji, nakushauri uuze vitu vingi ambavyo ulinunua ukiwa masomoni.
Anza kwa kuuza nusu ya nguo ulizonazo sasa, kwa sababu hutazivaa, pili uza smartphone uliyonayo sasa, ni ya gharama kubwa na kama mpaka sasa huna biashara haina msaada wowote kwako.
Ukipiga mahesabu ya haraka haraka unaweza kupata kiasi fulani cha fedha kinachotosha kuanzia kama utauza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa kwa sasa.
Kama nilivyosema hapo juu, tatizo kubwa sio mtaji bali mipango yako mwenyewe na kiasi gani unahitaji kuingia kwenye biashara.
Kama kweli unataka kuingia kwenye biashara, jipe mwaka mmoja tu wa kukusanya mtaji, katika mwaka huo, fanya kila kitakachopita mbele ya macho yako, ila kiwe halali kuweza kupata mtaji unaohitaji.
Kuendelea kulalamika kwamba kinachokuzuia ni mtaji hakutakusaidia chochote zaidi ya kuendelea kuwa na maisha magumu.
Anza sasa, asilimia tisini ya mtaji unaohitaji ni akili yako, anza kuitumia.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kupata mtaji wa kuanza biashara.

No comments:
Post a Comment