Tuesday, 12 April 2016

SHAMSA FORD KASEMA ALIACHANA NA NAY WA MITEGO KISA MANENO YA WATU ILA KWA SASA AKISEMA WARUDIANE YUPO TAYARI

LAYIII
Ukweli vigodoro haviwezi kuisha dar bonyeza picha hii kushudia vigodoro vingine huko bichi

Baada ya kauli ya rapa Ney wa Mitego kwa mpenzi wake wa zamani, Shamsa Ford kwamba kama anachagua wasichana wa kurudiana naye atakuwa wa kwanza kutokana na ukarimu na mapenzi yake, mrembo huyo ameibuka na kufurahia kauli hiyo.
Shamsa ambaye mara zote alikuwa amepambwa na Bashasha, alidai Penzi lake na rapa huyo lilivunjwa na maneno ya watu.

“Mimi na Ney tuliwahi kuwa wapenzi japo tumeachana ila kiukweli tulipendana sana na kama tutarudiana hakuna tatizo kwa kuwa nampenda sana.
“Tuliachana na Ney kutokana na maneno maneno ya watu waliokuwa hawapendi penzi letu, lakini kama anataka turudiane nipo tayari,” alijieleza Shamsa huku akifurahia kauli zake hizo.
Aliongeza kuwa yeye si mnafiki kwa alichonacho moyoni na hawezi kuongea kwa kashfa kama baadhi ya waigizaji wenzake wanapotofautiana ama kuachana na waliokuwa wapenzi au waume zao.
Shamsa Ford amewahi kutamba na filamu mbali mbali ikiwepo ‘Bado natafuta’ na ‘Chausiku’.

No comments:

Post a Comment

advertise here