Wednesday, 27 April 2016

MR BLUE NA ALIKIBA MBIONI KUACHIA MZIGO MKUBWA

LAYIII
Mr Blue kuachia Mkwaju na King Kiba.
Nota wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ ambaye hivi karibuni aliuaga ukapera kwa kuamua kufunga pingu za maisha na mzazi mwenzake, Wayda, amedai anatarajia kuachia wimbo mpya ambao amemshirikisha Ali Kiba.
Mr Blue amedai kwamba wimbo huo utajulikana kwa jina la ‘Mboga Saba’
Akizungumza na MTANZANIA, Mr Blue alisema kuwa wimbo huo upo tayari na anatarajia kuuachia wiki
ijayo endapo mtayarishaji wake, Man Water atamkabidhi.
“Kiukweli huu wimbo haujawahi kutokea na utakuwa bonge la wimbo kwa kuwa tumekutana wakali wa muziki, ninaamini wimbo huo utakuwa ni historia katika tasnia ya muziki hapa nchini,” alisema Mr Blue.
KUTANA NA ADAMORE HAPA 




No comments:

Post a Comment

advertise here