Rais wa Tanzania
John Magufuli amependekeza daraja mpya la Kigamboni lipewe jina la
mwanzilishi wa taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere.
Akiongea muda
mfupi kabla ya kuzindua rasmi daraja linafaa kupewa jina la Mwalimu
Julius Nyerere kutokana na mchango wake kwa nchi hiyo.
Daraja la
Kigamboni lilianza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 na lina urefu wa mita
680 na barabara unganishi upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu
wa kilomita 2.5.
Rais Magufuli baada ya kuzindua daraja la Kigamboni
Ujenzi wake ulifanywa na kampuni ya China Railway 15 Group ikishirikiana na kampuni ya China Bridge Engineering Group.
Daraja
hilo ndilo la kwanza la kubeba uzito wa barabara kwa kutumia nyaya
Afrika Mashariki na la tatu Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara bila
kuhesabu Afrika Kusini.
Linamilikiwa na serikali ya Tanzania na
Hazina ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) kwa 40% na 60% mtawalia na litachukua
nafasi ya feri ya MV Magogoni. Wenye magari watalipia kutumia barabara hiyo
Wenye magari na pikipiki watahitajika kulipa kutumia daraja hilo lakini wapitanjia watavuka bila malipo.
Ujenzi wa daraja hilo, ambao uligharimu dola 128 milioni za Kimarekani, ulianza mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment