Monday, 25 April 2016

CHANZO PICHA ZA UCHI SIWEMA WA NAY AFUNGWA MIAKA MIWILI ...NAY AAPA KUMTOA GEREZANI

LAYIII
siwema1
Wiki iliyopita zilianza kusikika taarifa mbalimbali kuhusu kuhukumiwa kwa mpenzi wa zamani na mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili  jijini  Mwanza.


Pamoja na taarifa zote hizo kutoka hakukuwa na taarifa za kina kueleza ni nini hasa kilitokea mahakamani mpaka akahukumiwa jela miaka miwili  ila taarifa za awali  zilidai kwamba
amehukumiwa kwa sababu ya kutukana mtu mtandaoni.


Wakili wa serikali Moris Mtoi ameongea kwenye exclusive interview na DStv  na kusema ukweli au chanzo cha Siwema kuhukumiwa hakikua kumtukana mtu mitandaoni bali kumtishia mtu.


Amesema kilichompeleka Siwema jela nikumtishia mpenzi wake wa zamani kutoa picha za uchi walizopiga, Siwema alikua akimtishia kwamba asingetoa pesa na kumnunulia gari au kufata maagizo yake angezisambaza picha hizo kwa mke wake na watu wengine.


Wakili huyu wa serikali na mwendesha mashtaka kwenye kesi hii amesema vitu vingine alivyokuwa akivitaka Siwema ni kununuliwa nyumba na boyfriend wake huyu wa zamani.

GLADNESS MALLYA
Roho inauma! Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa yupo kwenye harakati za kumsaidia mzazi mwenzake, Siwema Edson (27) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kujipatia mali kwa njia ya vitisho kutoka kwa kigogo mmoja serikalini aliyetajwa kwa jina moja la Deo.
Katika msala huo, Siwema alidaiwa kutoa vitisho kwa mlalamikaji akimtaka kumnunulia gari aina ya Honda CVR lenye namba za usajili T103 DDU lakini pamoja na kutimiziwa matakwa yake hayo, aliendelea kumtumia vitisho, akimtaka amtumie kiasi kikubwa cha fedha za mtaji, ndipo mlalamikaji akatoa taarifa polisi kisha mrembo huyo, akakamatwa ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita alitupwa jela.
Akipiga stori na gazeti hili mara baada ya hukumu kutolewa mwishoni mwa wiki iliyopita Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Nay alisema tayari ameshatafuta mawakili wawili kwa ajili ya kukata rufaa ili kama itawezekana mama mtoto wake huyo arudi uraiani.

JE UMEMISS KUONA MWONEKANO MPYA W DARAJA LA KIGAMBONI VIDEO HII HAPA

No comments:

Post a Comment

advertise here