Friday 15 April 2016

BOBOA BOMOA INAZIDI KUPIGWA KALENDA

LAYIII
Bomoabomoa iliyoanza mwishoni mwa mwaka 2015 kwenye maeneo mbalimbali ya mabondeni ikiwemo kwa maeneo yaliyo kando na mto msimbazi ambapo zoezi hilo lilisitishwa baada ya wakazi wa Tabata Segerea kufungua kesi kupinga ubomoaji wa nyumba zao. 
April 15 2016 ilikuwa ni siku ambayo kesi ilitakiwa kutolewa hukumu katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi lakini taarifa iliyotoka ni kwamba Jaji Fredrica Mgaya aliyetakiwa kusoma hukumu hiyo anaumwa. Wakizungumza na millardayo.com Diwani kata ya Tabata, Patrick Assenga na Mbunge wa viti maalum Segerea, Anatropia Theonest, wamesema …..

>>>’tumefika kama kawaida mbele ya jaji lakini kwa bahati mbaya tumeambiwa kwamba afya yake haijaendelea vizuri na badala yake imeahirishwa mpaka ijumaa ijayo April 22 tunaomba jaji aliyepewa hiyo kesi kama anaona hawezi kuhudhuria siku hiyo mahakama ipange mtu mwingine akatoe uamuzi wa kesi yetu kwa sababu tunaamini kila kitu kimekamilika’;-Anatropia Theonest
>>>’uamuzi unaweza kusomwa hata na msajili wa mahakama, kesi inapokuwa imekamilika katika hatua hii msajili wa mahakama peke yake anaweza kusoma huo uamuzi na sio issue kubwa, wakati mwingine unapoona mambo kama haya yanapelekea wananchi kuwa wasiwasi kuwa kesi inaingiliwa’:- Patrick Assenga

No comments:

Post a Comment

advertise here