LAYIII
Mkurugenzi
wa Straight up Vibes Omary Abood (wa kwanza kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya kumtambulisha rasmi Msanii
Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la
mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika
ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha
wa mwaka mpya.
Dj
rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru”
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya
kumtambulisha rasmi Msanii Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa
kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold
finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga
karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya. Dj huyo atasimamia
vilivyo kazi yake katika shughuli nzima ya Tamasha
hilo.
hilo.
Dj
rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru”
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla
iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya
kumtambulisha rasmi Msanii Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa
kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown and Sexy, the Gold
finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga
karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya. Dj huyo atasimamia
vilivyo kazi yake katika shughuli nzima ya Tamasha hilo.
Msanii
Tekno Miles (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa hafla iliyomtambulisha rasmi kwa waandishi wa
habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown
and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon
uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo
pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea
kuanzishwa kwake.
Meneja
Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija
(Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Tekno Miles (wa kwanza
kushoto) na Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young
Guru” wakati wa hafla iliyomtambulisha Msanii Tekno Miles kwa waandishi
wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown
and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon
uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo
pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea
kuanzishwa kwake.
---
Maandalizi
ya Tamasha maarufu la Johnnie Walker “Grown and Sexy The Gold finale”
kwa ajili ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya yanaendelea vizuri
ambapo kwa mujibu wa waandaaji wa Tamasha hilo, “Capital events” kupitia
wadhamini wao “Johnnie Walker” chapa maarufu ya pombe kali
inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti wamemleta Msanii Tekno
Miles kutoka Nigeria kutumbuiza laivu katika Tamasha hilo ambalo litakua
la mwisho kabisa katika historia ya matamasha ya Grown and Sexy nchini
Tanzania.
Akizungumza
wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika hoteli ya
Serena jijini Dar es salaam,Meneja chapa wa pombe kali SBL Shomari Shija
alisema, “Tumeamua kulidhamini Tamasha hili kama njia mojawapo ya
kujumuika na kufurahi kwa pamoja na wateja wetu wa chapa za Johnnie
Walker katika kuuaga rasmi mwaka huu wa 2015.
Bw.
Shija aliongeza kuwa katika Tamasha la mwaka huu ambalo ni la mwisho
katika historia ya mfululizo wa matamasha ya Grown and Sexy waliona ni
vema kumleta msanii maarufu toka Nigeria “Tekno Miles” ambaye aliwasili
jana usiku mida ya saa nane akitokea Nigeria tayari kwa kulipamba
Tamasha hilo. Msanii huyo ambaye anatamba na vibao mbalimbali kwenye
anga ya muziki hivi sasa kama Shoki, Duro na Wash atatumbuiza laivu
kwenye Tamasha hilo ambalo litafanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya
katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Msasani karibu na Best
Bite.
Sambamba
na uwepo wa msanii huyo wengine wataopamba Tamasha hilo ni Dj Maarufu
“Young Guru” ambaye ni Dj rasmi wa msanii Jay Z toka Marekani ambaye
ataisimamia shoo hiyo vilivyo pamoja na malkia wa uswazi mwanadada
“Shaa” kisura wa Tamasha hilo ambaye atasherehesha shughuli nzima katika
usiku wa tukio.
Kwa
upande wake Msanii Tekno alisema anafurahia kusherekea mkesha wa mwaka
mpya akiwa Tanzania na kuahidi kuporomosha burudani ya nguvu kwa
mashabiki wake watakaojitokeza kushuhudia Tamasha hilo la kufunga mwaka.
Naye
Mwakilishi wa Capital events waandaaji wa Tamasha hilo Bw. Justin
Massawe alisema “Tunawakaribisha wapenzi wote wa burudani na chapa ya
Johnnie Walker kujitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha letu la mwisho la
Grown & Sexy na kuahidi kuwa litakuwa la kufana zaidi kwani
wamejipanga kutoa burudani ya nguvu na kuwafurahisha mashabiki
mbalimbali.
“Ningependa
kuwashukuru wadhamini wetu mbalimbali katika kipindi chote cha
mfululizo wa matamasha haya tokea yalipoanzishwa rasmi kwa ushirikiano
mzuri ambao wametupatia hadi hii leo tunapofunga rasmi tamasha hili la
mwisho la Grown and Sexy the Gold finale.”
Bw.
Justin hakusita pia kuwashukuru Johnnie Walker kwa kuhakikisha
wanakamilisha mikataba yote ya kumleta msanii Tekno Miles pamoja na Dj
Young Guru hapa nchini na kwa kuhakikisha kwamba tamasha la mwisho
linakamilika kwa mafanikio” makubwa zaidi.
No comments:
Post a Comment