LAYIII
BONYEZA PICHA KUONA VIDEO YA NYANI ALIVYOKUWA AKIMBEMBELEZAA MMEWE
KUMBE HATA KWA WANYAMA
BONYEZA PICHA KUONA VIDEO YA NYANI ALIVYOKUWA AKIMBEMBELEZAA MMEWE
KUMBE HATA KWA WANYAMA
Wema
Sepetu ni bingwa wa kutumia gharama kubwa kufanya filamu na kutengeneza
kiu kubwa kwa mashabiki wake halafu then mradi unageuka kuwa kama album
ya Detox ya Dr Dre, ambayo haijawahi kutoka hadi leo.
June
2012: Muigizaji wa Nigeria, Omotola Jalade akiwa na Wema baada ya
kuwasili kutoka Nigeria kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Superstar
ambayo hadi leo haijatoka
Miaka
minne iliyopita, Wema alidai kutumia mamilioni ya shilingi kufanya
filamu aliyoipa jina ‘Superstar.’ Na hata uzinduzi wake uliofanyika
Hyatt Regency Hotel (Kilimanjaro) ulikuwa wa kifahari na wa aina yake.
Mastaa karibu wote wa Tanzania walialikwa na kuona sehemu ya filamu
hiyo.
Alitisha
zaidi kwa kumleta msanii nguli wa Nigeria, Omotola Jalade aliyeshuhudia
uzinduzi huo. Bahati mbaya hadi leo filamu hiyo haijawahi kutoka sokoni
na mrembo huyo aliamua kuifungia kabatini.
Tupeleke
mbele. Mwaka jana Wema alienda Ghana na kufanya filamu na staa wa huko,
Van Vicker iitwayo ‘Day After Death’. Filamu hiyo ilifanyika December
2014. Kwa mujibu wa ratiba ya mwisho, ilikuwa itoke September mwaka
jana.
Meneja wake, Martin Kadinda, alidai ilishindikana kutoka kwasababu ya kampeni za uchaguzi.
“Filamu
mpaka sasa ipo tayari, lakini movie hii hatuwezi kuiachia kama
anavyoachia movie nyingine.Lazima afanye launch na ilikuwa launch
ifanyike toka mwezi wa tisa lakini toka mwezi wa sita mpaka sasa Wema
yupo kwenye kampeni,” Kadinda aliiambia Bongo5.
“Kwahiyo
tunasubiri mpaka hizo kampeni ziishe na uchaguzi upite Wema atakuwa
anazindua products zake mpya halafu baada ya hizo products kuzinduliwa
ndio filamu itazinduliwa rasmi,” aliongeza.
Lakini
hadi sasa hakuna dalili za filamu hiyo kutokana na haiongelewi tena?
Kunani? Tuna wasiwasi kuwa filamu hii inaweza kuungana kabatini na
Superstar zikipeana moyo.
Bongo 5
No comments:
Post a Comment