Friday, 11 March 2016

KENYA NDANI YA DARUBINI YA IAAF

LAYIII
 Mkutano wa kamati kuu ya shirikisho la mchezo wa riadha duniani IAAF ambayo imekuwa ikikutana mjini Monaco imetangaza kuwa Kenya na Ukraine ni miongoni mwa nchi ambazo zimewekwa katika orodha ya mataifa ambayo yanachunguzwa kwa kina na shirikisho hilo kuhusiana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli michezoni.


Mataifa mengine ni pamoja na Ethiopia, Morocco, na Belarus
Kwenye kikao na waandishi wa habari, afisa mkuu wa shirikisho hio anayehusika na maadili amesema kuwa, mataifa hayo yamepewa muda kuunda kamati maalum, ili kudhibiti matumizi ya dawa hizo michezo.

kuhusu Urusi, ambayo imepigwa marufuku kushiriki katika mashindano yoyote ya kimataifa, shirikisho hilo limesema kuwa uamuzi utachukulia mwaka huu,ikiwa taifa hilo litaruhusiwa kushirika katika mashindano ya Olimpiki mjini Rio nchini Brazil.
IAAF imesema kuwa Urusi haijatekeleza masharti yote yaliyowekwa ili marufuku hiyo kuondolewa.
Urusi na shirikisho la riadha nchini humo zimetuhumiwa kuhusika na ufadhili wa utumizi wa dawa za kusisimua misuli michezoni na kuficha ukweli kuhusu wanariadha wake.
Chanzo na BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

advertise here