LAYIII
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Samatta January 29 taarifa za yeye kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji zilianza kuenea, na baadae kuthibitika baada ya picha za utambulisho wa staa huyo kuanza kuenea mitandaoni.
Huenda ilikupita au ulipata nafasi ya kutazama sehemu ndogo ya utambulisho wa Mbwana Samatta ambaye wengi tuliona akitambulishwa na kukabidhiwa jezi namba 77 tukiwa hatujui kwa nini kachagua jezi hiyo, Samatta ameeleza sababu ya kuchagua kuvaa jezi hiyo.
“Nimechagua
jezi namba 77 kwa sababu wachezaji niliokuwa nawapenda mimi kama akina
Eric Cantona, Cristiano Ronaldo na David Beckham walikuwa wanavaaa jezi
namba 7, Mr Dimitri alivyoniuliza napenda kuvaa jezi namba ngapi
nilimwambia jezi 77 kwa maana sikutaka kugombania namba ya jezi, kwa
kila klabu unayokwenda ni ngumu kukuta jezi namba 7 haina mtu, sasa
sikutaka kugombania namba ya jezi lakini mimi pia ni shabiki wa Man
United” >>> Samatta
Video ya utambulisho na interview ya Samatta baada ya kutua KRC Genk
No comments:
Post a Comment