LAYIII
BONYEZA PICHA KUIONA VIDEO
Stori: Joseph Ngilisho, Ijumaa
Arusha: Ukatili wa watoto haukubaliki! Mama mzazi aliyetajwa kwa jina moja la Anna, mkazi wa Oysterbay maeneo ya Unga-Limited jijini hapa anadaiwa kumcharanga kwa viwembe mwanaye wa kumzaa mwenye umri wa miaka kumi anayesoma shule ya msingi (jina la mtoto na shule yanahifadhiwa).
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri mapema wiki hii nyumbani kwa mama huyo maeneo ya Oysterbay hivyo kumlazimu Diwani wa Kata ya Themi, Melance Kinabo kushirikiana na polisi kumkamata mzazi huyo kutokana na kitendo alichomfanyia mwanaye na kumwachia majeraha makubwa.
Kwa mujibu wa mshuhuda wa tukio hilo, mama huyo anayefanya kazi kwenye moja ya viwanda vilivyopo Unga-Limited, anadaiwa kumfanyia mwanaye ukatili huo huku kisa kikielezwa ni kitendo cha mtoto huyo kukataa kuchota maji.
Ilielezwa kuwa, mtoto huyo kwa sasa anapatiwa matibabu kwenye zahanati moja iliyopo Unga-Limited jijini hapa kufuatia majeraha ya kutisha ya viwembe kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake hasa mapajani.
Habari za kipolisi zilieleza kwamba, baada ya mama huyo kushikiliwa polisi alikiri kumwadhibu mwanaye huyo kwa kushindwa kwenda kuteka maji bombani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Liberatus Sabas hakuweza kupatikana kufuatia simu yake kutopatikana.
TIZAMA VIDEO JINSI MKONO WA HUYU DADA ULIVYOKOSWA KOSWA NA PAPA

No comments:
Post a Comment