Sunday 21 February 2016

SHILOLE ALEWESHA DOGO MAPENZI AMBEMENDA OVYO OVYO

LAYIII

IMG_9282Msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ akipozi kimahaba na Medy Music.
Stori: Musa mateja, Ijumaa:
Dar es Salaam: Baada ya msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kumwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, hivi karibuni Ijumaa lilinyetishiwa kuwa, amejiweka kwa dogo mmoja aliyefahamika kwa jina la Medy Music ambaye wamekuwa wakipika na kupakua kwenye nyumba ya staa huyo iliyopo Kijitonyama jijini Dar.

Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu juzikati jioni alitinga nyumbani kwa Shilole na kufanikiwa kuwakuta wawili hao lakini katika hali ya kushangaza, baada ya kuona kamera wakaanza kufanyiana vituko vya kimahaba.
BONYEZA PICHA HIII KUONA VIDEO
IMG_9308
wakifuatilia jambo kwenye simu.
Shilole alionekana kumshikashika Medy huku dogo huyo aliyeonekana kuwa kama kalewa akitoa ushirikiano.Katika meza iliyokuwepo sebuleni kulikuwa na chupa za bia lakini mara kadhaa Shilole alionekana akinywa juisi huku dogo akipiga maji, mazingira yaliyoonekana kuwa Shilole alikuwa akimlewesha kwa makusudi kisha mambo ya ‘kuchi…kuchi’ yachukue nafasi.
Akizungumzia uhusiano wake na Medy, Shilole alikiri kuwa ndiye mpenzi wake kwa sasa na akawataka wanaodai anambemenda wakidhani ni mtoto wakae kimya.“Huyu ndiye laazizi wangu kwa sasa, ana kila sifa ya kuwa mume wangu na wala siyo mtoto, ni mtu mzima kabisa tofauti na Nuh,” alisema Shilole kisha kuendelea kumdekea jamaa huyo aliyeonekana kafa-kaoza kwa staa huyo.
Wakati Shilole akifanya yake, Nuh naye juzikati alitupia picha kadhaa mtandaoni akiwa kimahaba na demu mkali aliyefahamika kwa jina la Erah Erah anayedaiwa kuwa mpenzi wako
CHUKUA MUDA WAKO KUITAZAMA HII VIDEO YA HAWA JAMAA WALIOJIFANYA VIPOFU KISA MWANAMKE


No comments:

Post a Comment

advertise here