LAYIII
Kwa kawaida maandalizi ya Michuano ya Kombe la Dunia
hufanyika miaka zaidi ya minne kabla ya nchi husika kuanza kupokea timu
katika miji yao. Imekuwa kawaida kwa kila nchi inayotarajia kuwa
mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia kutengeneza viwanja vipya na
vyenye hadhi kwa ajili ya michuano hiyo.
Nchi ya Qatar ambayo ndio mwenyeji wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022 mtandao wa sokka.com
umetoa list pichaz 12 za viwanja vinavyotajwa kuwa vitatumika katika
mihuano hiyo 2022. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee pichaz 12 za
muonekano wa viwanja 12 vilivyotajwa na sokka.com
kuwa vitatumika 2022.
1- Lusail Iconic Stadium
Huu
upo mji wa Al-Daayen na unamilikiwa na kamati ya Olympic ya Qatar na
una uwezo
wa kuchukuwa mashabiki 86,250, utattumika katika mechi za
makundi ya michuano
hiyo, 16 bora, robo fainali, nusu fainali na
fainali.
2- Khalifa International stadium
Upo
mji wa Al-Rayyan na unamilikiwa na serikali na kamati ya Olympic
unauwezo wa
kuchukua mashabiki 50000. Utatumika katika mechi za makundi,
16 bora, robo fainali
na nusu fainali.
3- Sports City stadium
Utachezewa mechi za makundi na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu upo mji wa Doha
na unauwezo wa kuchukua mashabiki 47,560.
4-Al-Khor Stadium
Hiki
pia kinamilikiwa na serikali pamoja na Qatar Olympic Committee kipo mji
wa
Al-Khor kitatumika kuchezea mechi za makundi na 16 bora pia kina
uwezo wa kubeba
mashabiki 45,330.
5-Al-Shamal Stadium
Huu
utachezewa mechi za hatua ya makundi lakini unamilikiwa pia na Serikali
ya Qatar
pamoja na Qatar Olympic Committee. Upo mji wa Al-Shamal
unauwezo wa kuchukua
mashabiki 45,120.
6-Al-Wakrah Stadium
Mji
wa ambao Al-Wakrah upo uwanja huu utapata nafasi ya kuona mechi za
makundi na 16 ya
michuano hiyo. Unamilikiwa na Serikali ya Qatar na
Qatar Olympic Committee ukiwa
na uwezo wa kuchukua mashabiki 45,120.
7-Umm Slal Stadium
Mji
wa Umm Slal utapata nafasi ya kushuhudia mechi za makundi, 16 bora na
robo
fainali zitakazochezwa katika uwanja huo. unamilikiwa na serikali
ya Qatar
na unauwezo wa kuchukua
mashabiki 45,120.
8-Doha Port Stadium
Mji
wa Doha ndio kipo kiwanja hiki kinachomilikiwa na Serikali ya Qatar
kitatumika
katika mechi za makundi, 16 bora na mechi za robo fainali.
kinaripotiwa kuwa na uwezo
wa kubeba mashabiki 44,950.
9- Education city stadium
Hiki
ni kiwanja kingine kilichopo Al-Rayyan Qatar ambacho kitatumika katika
michuano
hiyo. Uwezo wake wa kuchukua mashabiki ni 45,350.
10-Al-Gharafa Stadium
Kipo mji wa Al-Rayyan na kitatumika katika mechi za hatua ya makundi pekee. Uwezo
wa kuchukua mashabiki ni 21,282.
11-Al-Rayyan Stadium
Hiki
ni kiwanja kingine kitakachotumika katika michuano hiyo kipo katika mji
wa
Al-Rayyan, huu ni uwanka ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua
mashabiki 21,282.
12- Qatar University Stadium
Doha kutakuwa na uwanja mwingine utakaotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2022
ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 43,520.
No comments:
Post a Comment