LAYIII
Headlines za beef kati ya rapper Lil Wayne na Boss wa Cash Money Records Birdman ni miongoni mwa stori zilizokaa kwenye kurasa za burudani kwa kipindi kirefu, lakini baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya wawili hao, Lil Wayne maarufu pia kama Birdman Jr na Birdman wamefikia muafaka wa ugomvi wao tarehe 17 January 2016 maeneo ya LIV Nightclub, Miami.
Licha ya kesi yao kuendelea Mahakamani, Boss wa CMR, Birdman alichukuwa time kuwaambia watu waliokuwepo kwenye club hiyo kuwa uhusiano wake na Lil Wayne utabaki kuwa imara…
>>>”Huyu
ni mwanangu, na nipo radhi kufa kwa ajili yake na kuishi kwa ajili
yake, na ninaweza hata kuua kwa ajili yake, mmeniskia? Hii hakitakuja
kubadilika. Ni YMCMB for life!!” <<<< Birdman alisema.
Lil Wayne hakusema
chochote bali kutoa tabasamu na baada ya hapo wawili hao walipiga toast
ya Champagne na kisha kuperform collabo yao ya mwaka 2006, ‘Stuntin Like My Daddy.’ Drake
amabaye pia alikuwepo kwenye club hiyo alichukua time kupost picha ya
tukio hilo kwenye page yake ya Instagram na maneno yaliosema; “Together we stand, Divided we fall”.
Unaweza kutazama tukio zima hapa chini kwenye hii video.
No comments:
Post a Comment