Saturday, 16 January 2016

HAWA MASTAA NA HAKA KAMCHEZO KUNA NINI?

LAYIII


wema-auntWema Sepetu na Aunt Ezekiel
Miongoni mwa mastaa wa filamu na muziki Bongo wamekuwa na viashiria vya vitendo visivyofaa hasa wanapokuwa kwenye sehemu za starehe na wengi wao ni wale wanaotumia kinywaji chenye kilevi.
Wanaotajwa sana kwenye tabia hiyo mni pamoja na hawan wafuatao kutokana na picha zao kuzagaa nsana mitandaoni na kwenye magazetin mbalimbali.
Hapa nawazungumzia Aunt Ezekiel na Wema Sepetu, Isabela Mpanda na Baby Madaha, Rayuu na Skaina nk.

Mastaa hawa kwa nyakati tofauti wamekuwa wakionesha wazi viashiria hivyo kwa kupigana picha na picha hizo kuzagaa kwenye vyombo vya habari.
Wao kwao imekuwa kama fasheni na muda mwingi hulichukulia suala hili kama la kawaida kwa madai kuwa ni kutokana na ukaribu wa urafiki walionao.
rayuu na skainaSkaina na Rayuu
Je, kabla ya ustaa walikuwa wakisalimiana na kuwa karibu hivi?
Ni swali ambalo linaulizwa na kila msomaji pengine na hata wazazi wanaowazunguka kwani kwao ni vitu vigeni.
Ustaa ndiyo shinikizo la viashiriahivi ama veepe?
Wasanii wengi wanapokuwa wameshaingia kwenye tasnia ndiyo huanzisha mambo ya ajabu na wengine hudiriki kujifunza tabia ambazo hawakuwa nazo kabla.
bella-na-madahaaBela na Baby Madaha
Imefikia hatua ya wazazi kushindwa kuwaingiza watoto wao kwenye tasnia hususan Bongo Muvi kutokana na jinsi wengi wao wanavyoharibiwa na mchanganyiko wa watu wanaokutana nao.
Ni ustaa ama veepe, kwani kila anayeonekana akimbusu mwenzake lazima liwe busu lenye viashiria vya vitendo vichafu.
Swaga hii ya mabusu ilianzia kwa mastaa wakubwa, Aunt Ezekiel na mwenzake Wema Sepetu sasa imekuwa kama mtindo kwa mastaa wanaotoka.
Hivi hamuoni kuwa nyie ni chanzo cha mastaa wajao kuharibika? Busu hili si utamaduni wetu Watanzania na mbaya zaidi hufanya kitendo hicho baada ya kulewa.

1 comment:

advertise here