LAYIIII
BONYEZAPICHA YOYOTE ITAKUPELEKA MOJA KWA MOJA KATIKA TUKIO NZIMA
BONYEZAPICHA YOYOTE ITAKUPELEKA MOJA KWA MOJA KATIKA TUKIO NZIMA
Musa Mateja ASANTE
Mungu! Mume wa muimba Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameangusha
bonge la pati nyumbani kwake Tabata Kimanga Mwisho, jijini Dar, Jumapili
iliyopita kama shukrani kwa Mungu kwa kumfanikisha kushinda kesi ya
ubakaji iliyokuwa ikimkabili.
ANGALIA VIDEO JINSI NGUVA ALIVYO TAFUNA MKONO WA ALIYE MFUGA
Akizungumza na gazeti hili nyumbani
kwake siku ya tukio, Mbasha alisema kwamba anamshukuru sana Mungu kwani
katika kipindi ambacho kesi hiyo ilivyokuwa mahakamani, hakuwa na furaha
na muda wote alikuwa akimuomba Mungu aweze kumnusuru na kifungo.
JINSI NGUVA ALIVYO TAFUNA MKONO WA ALIYE MFUGA
ANGALIA VIDEO JINSI NGUVA ALIVYO TAFUNA MKONO WA ALIYE MFUGA
Mbasha ambaye alikuwa akikabiliwa na
kesi ya kumbaka shemeji yake nyumbani kwake, mwaka jana kipindi
alichokuwa akiishi na mkewe, amesema kitendo cha yeye kuwa uraiani ni
jambo la kumshukuru Mungu na ndiyo maana akaamua kuchinja ng’ombe
kuwaalika ndugu jamaa na marafiki wale pamoja.
“Nina furaha mno, siwezi kuizungumzia
furaha yangu lakini Mungu Baba wa Mbinguni ananijua ni jinsi gani
nilivyofurahi moyoni mwangu kwani kipindi ambacho nilikuwa nikisimama
mahakamani, niliiona kabisa milango ya jela mbele yangu,” alisema
Mbasha.
Katika sherehe hiyo, waalikwa walikula hadi kusaza na kumshukuru Mbasha kwa kuiandaa.
“Tunamshukuru sana. Tumekula na kunywa
hadi tumebakiza vingine, Mungu ni mwema, tunamuombea Mbasha azidi
kufanikiwa katika maisha yake,” alisema mmoja wa waalikwa ambaye
hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
No comments:
Post a Comment