Monday, 5 October 2015

WAKATI TUKITARAJIA ROBERTO KUFANYA COLLABO BONGO......NEY WA MITEGO YAMEMKUTA MENGINE KWAKE

LAYIII
Tanzania ilipata ugeni wa msanii kutoka Zambia Roberto aliyeimba ngoma ya ‘Amarula’ ambaye alikuja na kupiga show Mwanza..msanii Galaxy kutoka Tanzania amemshawishi Roberto wapige naye collabo moja..Galaxy amesema amepata connection nzuri ya kuweza kukutana na msanii huyo lakini bado hawajafanya collabo, kwa sasa tayari wamepanga mikakati yao na anachosubiri ni yeye awe tayari.
galaxy
Galaxy
Ney wa Mitego alivamiwa na majambazi nyumbani kwake Mbezi ya Kimara..Anasema siku ya tukio yeye hakuwa nyumbani na majambazi hao walifika nyumbani kwake majira ya saa 4 usiku..walikuja
na gari nyeusi aina ya landcruiser na kuanza kukata nyaya lakini wakazidiwa na majirani na baadaye wakakimbia.
house
Nay wa Mitego akiwa katika moja ya nyumba zake
Kundi la T Tanzania wamefanikiwa kushinda katika shindano la kudanse lililofanyika Kenya.. wamesema mashindano hayo yalifanyika wiki iliyopita Kenya na wamefanikiwa kushika nafasi ya kwanza..mashindano hayo yalianza mwaka jana ambapo walishiriki na kushika nafasi ya tatu… yameshirikisha nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

No comments:

Post a Comment

advertise here