Thursday, 22 October 2015

NAPE APATA AJALI MBAYA LINDI

LAYIII

Muonekano wa gari ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, Toyota Land Cruiser baada ya kupata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.

Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye.
...Gari hilo kwa mbele.

Gari la Nape likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali hiyo.
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amepata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.
Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi  alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.
Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo  ila anaendelea vizuri.
Akizungumza na GLOBAL PUBLISHERS LTD, Nape amesema: "Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima.
Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na 'air bag' nazo zimenisaidia."
Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.

No comments:

Post a Comment

advertise here