Monday 26 October 2015

MANENO YA KAMANDA KOVA JUU YA USAMBAZWAJI WA MATOKEO YA UCHAGUZI YASIYO HALAI

LAYIII
Tukiwa bado tunaendelea na Uchaguzi Mkuu kumekuwa na matukio mbalimbali yanayojitokeza kama kuenea kwa taarifa za washindi wa wagombea kutoka sehemu mbalimbali, sasa kamanda wa polisi wa kanda maalum, Suleiman Kova amezungumza na waandishi wa habari kuhusus na matukio hayo
Jambo tunalolipiga vita ni mtu nje ya tume kutangaza matokeo, hiyo ni dalili kubwa ya fujo. Tume ndio kisheria wamepewa kazi ya kutangaza matokeo‘- KAMANDA KOVA
Tunatoa onyo kwa mtu yoyote asivunje sheria hiyo, tuna idadi ya watu zaidi ya 100 tumekwisha wakamata ambao wamekuwa wakirekodi matukio mbalimbali ya uchaguzi nakuwasiliana na vyombo vya habari,  Huo ni uvunjifu wa amani‘- KAMANDA KOVA


No comments:

Post a Comment

advertise here