Thursday, 1 October 2015

ALIENS WATENGENEZA NDEGE KAMA SAHANI

LAYIII
Wiki iliyopita nilianza kuliangalia Eneo la Area 51 ambalo linahusishwa na hawa viumbe wa ajabu waishio angani wa Aliens. Eneo hili lipo katika Jimbo la Nevada nchini Marekani ambapo kama ilivyokuwa kwa Bermuda Triangle, nalo limejaa mauzauza ya kila aina. SASA ENDELEA…
Japo ni siri kubwa lakini inaaminika kuwa wapo Aliens wanaoishi eneo hilo ambalo lina ngome kubwa ya kijeshi ambayo mlango wake wa kuingilia umetengenezwa kamba pyramid (pembetatu) na ambao umechongwa kwa alama ya jicho moja. Kuhusu uwepo wa hawa Aliens eneo hili ndipo yanapoibuka maswali mengi hasa njia ya mawasiliano wanayotumia kwa maana ya lugha au ishara.

Katika eneo hili mambo mengi ya kiteknolojia yamekuwa yakishuhudiwa na watu waishio jirani na eneo hilo.
Kuna majengo ya ajabu ambayo ndani yake haijulikani kuna nini. Inaaminika hapo ndipo Aliens hubadilishana teknolojia na Wamarekani. Kivipi?
Wapo wanaoamini kuwa Aliens ndiyo huwaongoza majasusi wa Kimarekani hasa wanapokuwa kwenye jambo au jaribio la uvumbuzi wa teknolojia mpya ya anga.
Inasemekana kwa sasa bado wapo kwenye mpango wa kujaribu kutengeneza kiumbe chenye mchanganyiko wa binadamu na Aliens kwa sababu hawawezi kuingiliana na kuzaliana na binadamu.
Ishu nyingine kubwa ni kwamba watu wamekuwa wakijiuliza hawa Aliens huwa wanakula chakula gani?
Kuna andiko linaloonesha kuwa Aliens walitua eneo hili wakitokea kwenye Sayari ya Mars lakini hakuna uthibitisho kamili wa kile kinachosemwa.
Lakini bado ishu imekuwa ni ileile kwamba, viumbe hawa wana teknolojia ambayo inawawezesha kutengeneza ndege dizaini ya sahani. Inasemekana kwamba, kwa sasa hata Wamarekani nao wanatengeneza ndege za dizaini kama hii.
Maelezo mengine yanasema kwamba, viumbe hawa wanapatikana kilometa kama 150 kutoka Area 51 ambako inasemekana kwamba hakuna binadamu wa kawaida ambaye alishawahi kuingia ndani kabisa na siyo kusimama kwa mbali kisha akatoka akiwa hai. Hata mwandishi mmoja wa habari aliyerekodi video kwa mbali, alipotoka tu akaelezea aliyoyaona, alifariki dunia hapohapo.
Kinachofanyika ni kwamba, Marekani huwa wanatumia mitambo maalum ya kujilinda wakati wakiingia ndani na picha zinazopatikana huwa zipo chini ya uangalizi wa FBI (Federal Bureau of Investigation-Shirika la Upelelezi la Marekani) na sasa Marekani wanachukua kwa kasi Teknolojia ya Aliens (Aliens Software).
Inasemekana kinachowavutia Wamarekani ni kwamba, hawa Aliens wako mbali sana kimaendeleo. Wanafanya wanavyotaka na kuna stori kuwa binadamu wa kawaida duniani hawajaendelea kuweza kushirikiana kwenye jambo lolote.
Inadaiwa kuwa Aliens wakishirikiana na majasusi hao kwenye eneo hilo huweka mitambo mipya mara kwa mara ili kuzidi kujiimarisha.Inaelezwa kwamba, siyo rahisi kusikia stori kuwa watu wameona ndege ya ajabu sehemu nyingine duniani kama Afrika lakini mahali kama Area 51, Marekani, Uingereza na Urusi kila mwezi kuna ‘mavitu’ yanapaa hewani na hayatambuliki na yanaenda kwa spidi ya kasi sana na kupiga kona ya digrii 90 kwa spidi kali sana ikiaminika kuwa dunia hii hatuna teknolojia ya kufanya hivyo.
Hata hivyo, vyombo vyao vya anga pia hutokea kwa sekunde kadhaa na kupotea angani ikiaminika kuwa hawa Aliens ni viumbe ambavyo vinavyoweza kucheza na safari za masafa marefu angani kama mwendo wa mwanga. Safari ya miaka 200, wao wanaweza kutumia saa chache. Kumbuka mwanga husafiri kilomita milioni 1,076 kwa saa.
Juu ya UFO zinazoonekana eneo hilo, wataalam wanadai kuwa watu wanaishi jirani na eneo hilo wamekuwa wakipotoshwa na inawezekana wakaona ndege za kivita za kutisha tofauti na hizi za kawaida hivyo hudhani kuwa ni Aliens au UFO.
Itaendelea wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment

advertise here