Wednesday, 30 September 2015

MILIONEA ALIYEKIJENGA KISASA KIJIJI ALICHOZALIWA

layiii
ImageProxy
Milionea Xiong Shuihua akijisomea
ImageProxy (1)
Kijiji cha Xiongken, kusini mwa China alikozaliwa milionea huyo.ImageProxy (2)
Nyumba za kijijini hapo.ImageProxy (3)
Ujenzi uliofadhiliwa na Milionea Xiong katika kijiji cha Xiongken.ImageProxy (4)
Kijiji cha Xiongken baada ya kujengwa upya.ImageProxy (5)
Mitaa ikiwa katika muonekano mpya.ImageProxy (6)ImageProxy (7)
Miundo mbinu ikiwa imeimarishwa. ImageProxy (8)Wanakijiji wa Xiongken wakila chakula cha pamoja.ImageProxy (9)
Kijiji cha Xiongken katika muonekano mpya.
XIONG SHUIHUA (54) ambaye alizaliwa katika kijiji kiitwacho Xiongken, kusini mwa China, hivi karibuni aliamua kukijenga upya kijiji alichozaliwa na kukulia kama shukurani kwa wakazi wake ambao alikuwa nao wakati wa nyakati ngumu za umaskini, kabla hajapata utajiri.
Mtu huyo ambaye sasa ni milionea kutokana na biashara ya viwanda vya chuma,  aliamua kurejea katika kijiji chake hicho cha nyumbani kwao ambako kulikuwa na vibanda na nyumba chafu walizokuwa wanaishi wanakijiji wake.
Njia za kijiji hicho zilikuwa zimejaa uchafu na marundo ya taka kila mahali.  Hivyo Xiong alipoyaona yote hayo aliamua kuyabadili maisha ya wakazi wa kijiji hicho.
"Nilipata fedha nyingi ambayo nikashindwa kufahamu nitaitumiaje, hivyo nikakumbuka nilikotoka, nikaamua kuwasaidia watu wote walionisaidia mimi na familia yangu nilipokuwa mdogo,” anasimulia.
Hivyo, alivibomoa vibanda vyote na kujenga maghorofa ya kisasa na akajenga barabara mpya sehemu zilizokuwa na njia chafu na kulifanya eneo hilo kuwa la kisasa.
Isitoshe, milionea huyo mkaribu akamua kuwapa wazee na familia zenye vipato vya chini, milo mitatu ya bure kila siku.
Kutokana na ukarimu huo, hivi sasa familia 72 zinaishi katika nyumba za kisasa  na familia zingine 18 ambazo zilimsaidia sana, zilijengewa nyumba mpya, kubwa kila moja ikiwa ni baada ya kuishi katika mabanda ya miti kwa miaka nenda-rudi.
Mzee mmoja aitwaye Qiong Chu (75) alisema: “Nakumbuka wazazi wa Xiong walikuwa ni wakarimu kwa watu wote, ni jambo jema kwamba mtoto wao amerithi ukarimu huo.”

No comments:

Post a Comment

advertise here